METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 23, 2022

HALMASHAURI YA MKALMA YAFANIKIWA KUIFANYIA SENSA JAMII YAWAHADZABE BAADA YA KUWAPATIA NYAMA YA NG'OMBE


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Mesos akizungumza na viongozi wa Jamii ya Wahadzabe baada ya kufanikisha zoezi la sensa katika kijiji cha Midibwi katika halmashauri hiyo mapema hii leo agosti 23 2022


Karani wa Sensa akiwapokea taarifa za mkuu wa kaya wakati anatekeleza zoezi hilo kwenye familia za wahadzabe wilayani Mkalama.

Watoto wa jamii za Wahadzabe wakifurahia baada ya kula nyama ilioandaliwa ili wazazi wao washiriki zoezi la sensa

Taswira ya Nyama zilizofanikisha zoezi la sensa kwa wahadzabe katika halmashauri ya Mkalama Singida  



Karani wa sensa akimdodosa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mkalama Asia Mesos akiwa Nyumbani Kwake mapema asubuhi ya tarehe 23 agosti 2022.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo ambaye ni Mkuu wa kaya akijibu maswali katika dodoso la jamii nyumbani kwake.



Viongozi wa Halmashauri ya Mkalama wakiongoza na Mkurugenzi Asia Mesos wa tatu kutoka kushoto  wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanikisha zoezi la sensa kwa wahadzabe.

Mwenyekiti wa jamii ya Wahadzabe Wilaya ya Mkalama Edward Mashimba akiwatoa maelezo kwa Mkururugenzi wa Halmashauri ya Mkalama.


Na Hamis Hussein -Singida

Mkuu Wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida Sophia Mfaume Kizigo amesema wananchi Wa Wilaya hiyo wanapaswa kuendelea  kutoa taarifa zote sahihi zikiwemo za watu wenye makundi maalum ili kufanikisha zoezi la sensa linaloendelea nchini.

DC Kizigo amesema hayo agosti 23 mwaka huu 2022  baada ya kuhesabiwa akiwa nyumbani kwake ambapo amesema zoezi la sensa katika Wilaya hiyo limeenda kama walivyolipangilia.

Amesema zoezi hilo saa 6: 00 usiku Wa kuamkia Leo ambapo makundi yaliyofikiwa ni pamoja na mahabusu, Watoto Wa mtaani,wagonjwa Wa mahospitali .

"Zoezi la sensa katika Wilaya yetu limeenda vizuri sana, tumeanza saa 6 usiku Wa kumkia Leo tarehe 23 tumehesabu watu Wa makundi maalum wakiwemo Mahabusu,watoto Wa mtaani, wagonjwa wamahospitalini na familia mbalimbali tunawashukuru makarani wetu kwa kufanya kazi nzuri na tunawaomba waendelee mpaka zoezi Lita kapok familia" Alisema Dc Kizigo

DC Kizigo amesisitiza kwa kuwazitaka familia ambapo azitafikiwa na makarani siku ya Leo kutunza taarifa zao sahihi ili makarani watakapo wafikia ili kufanikisha zoezi hilo.

"Nitoe wito kwa wananchi wote ambao hawatafikiwa na makarani Leo basi watunze taarifa zao ili kukamilisha zoezi hili muhimu kwa ustawi wa taifa letu". Alisema DC Kizigo

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Juma Mesoss akiwa katika kijiji cha Midibwi kitongoji cha kipamba  amesema zoezi la kuhesabu familia za jamii ya Wahadzabe limefanikiwa kwa asilimia mia moja Mara baada ya kutenga bajeti ya kuwatafutia nyama jamii hio ambao inaishi kwa  kutegemea uwindaji,asali, matunda na mizizi ya porini.

"Tunashukuru tumefika katika kitongoji hiki cha Kipamba hapa Mkalama, kuangalia zoezi hili la sensa linavyoenda tuliona kuwa jamii hiii inategemea sana nyama na asali tukaona tutenge bajeti ambapo tumewapatia ng'ombe na wamesabiwa kisha wakala nyama zoezi limefanikiwa kwa aslimia 100%." Alisema Mkurugenzi huyo Asia 

Alisema jamii hiyo ya Wahadzabe inaishi kwa kutegemea uwindaji na asali  mizizi na matunda pori hivyo waliamua kuwapatia nyama ili wabaki kuhesabiwa majumbani mwao.

"Jamii hii inajihusisha na uwindaji  ni watu ambao hawatunzi chakula wala  hawalimi kwahiyo tumeona tulete nyama ambacho ndio chakula chao ili kufanikisha zoezi hili muhimu kwa ustawi Wa serikali yetu". Aliongeza Asia

Baadhi ya wananchi ambao ni jamii ya Wadzabe wameshukuru serikali ya halmashauri ya mkalama kwa kuwafanyia zoezi la sensa  pamoja na kuwapatia nyama na kuiomba serikali kuwasaidia kulinda utamaduni wao pamoja na kuwapatia Huduma za kijamii.



Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com