Karani wa Sensa akiwapokea taarifa za mkuu wa kaya wakati anatekeleza zoezi hilo kwenye familia za wahadzabe wilayani Mkalama. Watoto wa jamii za Wahadzabe wakifurahia baada ya kula nyama ilioandaliwa ili wazazi wao washiriki zoezi la sensa Taswira ya Nyama zilizofanikisha zoezi la sensa kwa wahadzabe katika halmashauri ya Mkalama Singida
![]() |
Karani wa sensa akimdodosa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mkalama Asia Mesos akiwa Nyumbani Kwake mapema asubuhi ya tarehe 23 agosti 2022. |
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo ambaye ni Mkuu wa kaya akijibu maswali katika dodoso la jamii nyumbani kwake. |
![]() |
Viongozi wa Halmashauri ya Mkalama wakiongoza na Mkurugenzi Asia Mesos wa tatu kutoka kushoto wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanikisha zoezi la sensa kwa wahadzabe. |
Mwenyekiti wa jamii ya Wahadzabe Wilaya ya Mkalama Edward Mashimba akiwatoa maelezo kwa Mkururugenzi wa Halmashauri ya Mkalama. |
Na Hamis Hussein -Singida
Mkuu Wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida Sophia Mfaume Kizigo amesema wananchi Wa Wilaya hiyo wanapaswa kuendelea kutoa taarifa zote sahihi zikiwemo za watu wenye makundi maalum ili kufanikisha zoezi la sensa linaloendelea nchini.
DC Kizigo amesema hayo agosti 23 mwaka huu 2022 baada ya kuhesabiwa akiwa nyumbani kwake ambapo amesema zoezi la sensa katika Wilaya hiyo limeenda kama walivyolipangilia.
Amesema zoezi hilo saa 6: 00 usiku Wa kuamkia Leo ambapo makundi yaliyofikiwa ni pamoja na mahabusu, Watoto Wa mtaani,wagonjwa Wa mahospitali .
"Zoezi la sensa katika Wilaya yetu limeenda vizuri sana, tumeanza saa 6 usiku Wa kumkia Leo tarehe 23 tumehesabu watu Wa makundi maalum wakiwemo Mahabusu,watoto Wa mtaani, wagonjwa wamahospitalini na familia mbalimbali tunawashukuru makarani wetu kwa kufanya kazi nzuri na tunawaomba waendelee mpaka zoezi Lita kapok familia" Alisema Dc Kizigo
DC Kizigo amesisitiza kwa kuwazitaka familia ambapo azitafikiwa na makarani siku ya Leo kutunza taarifa zao sahihi ili makarani watakapo wafikia ili kufanikisha zoezi hilo.
"Nitoe wito kwa wananchi wote ambao hawatafikiwa na makarani Leo basi watunze taarifa zao ili kukamilisha zoezi hili muhimu kwa ustawi wa taifa letu". Alisema DC Kizigo
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Juma Mesoss akiwa katika kijiji cha Midibwi kitongoji cha kipamba amesema zoezi la kuhesabu familia za jamii ya Wahadzabe limefanikiwa kwa asilimia mia moja Mara baada ya kutenga bajeti ya kuwatafutia nyama jamii hio ambao inaishi kwa kutegemea uwindaji,asali, matunda na mizizi ya porini.
"Tunashukuru tumefika katika kitongoji hiki cha Kipamba hapa Mkalama, kuangalia zoezi hili la sensa linavyoenda tuliona kuwa jamii hiii inategemea sana nyama na asali tukaona tutenge bajeti ambapo tumewapatia ng'ombe na wamesabiwa kisha wakala nyama zoezi limefanikiwa kwa aslimia 100%." Alisema Mkurugenzi huyo Asia
Alisema jamii hiyo ya Wahadzabe inaishi kwa kutegemea uwindaji na asali mizizi na matunda pori hivyo waliamua kuwapatia nyama ili wabaki kuhesabiwa majumbani mwao.
"Jamii hii inajihusisha na uwindaji ni watu ambao hawatunzi chakula wala hawalimi kwahiyo tumeona tulete nyama ambacho ndio chakula chao ili kufanikisha zoezi hili muhimu kwa ustawi Wa serikali yetu". Aliongeza Asia
Baadhi ya wananchi ambao ni jamii ya Wadzabe wameshukuru serikali ya halmashauri ya mkalama kwa kuwafanyia zoezi la sensa pamoja na kuwapatia nyama na kuiomba serikali kuwasaidia kulinda utamaduni wao pamoja na kuwapatia Huduma za kijamii.
0 comments:
Post a Comment