METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, July 15, 2022

TANZANIA SIO KAPU LA KUTULETEA DIGRII FEKI-WAZIRI MKENDA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa Prof Ndelilio Urio akimkabidhi zawadi ya picha Mgeni-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda wakati wa sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa iliyofanyika jana tarehe 14 Julai 2022 Mjini Iringa. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akisisitiza ulazima wa TCU kusimamia ubora wa elimu wakati wa sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa iliyofanyika jana tarehe 14 Julai 2022 Mjini Iringa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akiwa ameambatana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa Prof Ndelilio Urio wakikagua maktaba wakati wa sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa iliyofanyika jana tarehe 14 Julai 2022 Mjini Iringa.
Sehemu ya wanachuo na wakazi wa Iringa wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akihutubia wakati wa sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa zilizofanyika jana tarehe 14 Julai 2022 Mjini Iringa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akisaini kitabu cha wageni muda mchache baada ya kuwasili kwenye sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa ziliyofanyika jana tarehe 14 Julai 2022 Mjini Iringa.
Mgeni rasmi-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akipata maelezo ya kina kuhusu ufanyaji kazi wa kitengo cha TEHAMA wakati wa sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa iliyofanyika jana tarehe 14 Julai 2022 Mjini Iringa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa iliyofanyika jana tarehe 14 Julai 2022 Mjini Iringa.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa Prof Ndelilio Urio akimkabidhi zawadi ya picha Mgeni-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda wakati wa sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa iliyofanyika jana tarehe 14 Julai 2022 Mjini Iringa.
Mgeni rasmi-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Jimbo La Iringa Blaston Gaville wakati wa sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa iliyofanyika jana tarehe 14 Julai 2022 Mjini Iringa.

Na Mathias Canal, WEST-Iringa


Serikali imesema kuwa haitafanya uzembe kwenye usimamizi wa Ubora wa elimu nchini hivyo imeitaka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuhakikisha kuwa inaendeleza udhibiti wa ubora wa elimu nchini katika ngazi ya vyuo vikuu nchini.


TCU imekumbuswa lengo la kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja kuhakikisha inasimamia kwa weledi mkubwa elimu ya vyuo vikuu nchini kwa kufanya utambuzi na uidhinishaji wa elimu ya vyuo vikuu kabla ya chuo kikuu chochote kuanza.


Akizungumza jana tarehe 14 Julai 2022 wakati wa sherehe za siku ya Chuo Kikuu cha Iringa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amesema kuwa hakutakuwa na shinikizo lolote la utoajia wa Digrii zisizokidhi vigezo kwenye kazi za kitaaluma hivyo serikali itahakikisha kuwa ubora wa elimu unasimamiwa ipasavyo.


Waziri Mkenda amesema kuwa ili kuwe na wataalamu wazuri katika sekta ya afya ni vyema kama kuna uwezekano vigezo viongezwe hususani katika usimamizi wa maswala ya tiba ili kuakisi ubora wa elimu nchini.


"Tukicheza na ubora wa elimu tutaua nchi yetu, na hapa nchini vipo baadhi ya vyuo vya binafsi ambavyo ili viwe na wanafunzi wengi vinatoa GPA kubwa pasina kujali ubora na uwezo wa wahitimu wao" Amekaririwa Prof Mkenda na kuongeza kuwa


"Tanzania sio kapu la kutuletea Digrii feki hivyo ubora wa elimu utasimamiwa bila woga na presha ya watu wenye fedha au wana siasa, lakini na nyie TCU mtoe majibu kwa wakati mkichelewa hatutaelewana" 


Prof Mkenda amesema kuwa Vigezo vya udahili na utoaji elimu vinafahamika, ubora unafahamika, hivyo tathmini ikifanyika vikaangaliwa vigezo kila mtu atapata kwa mujibu wa vigezo hivyo na si vinginevyo.


"Nchi yetu haiwezi kuendelea kwa kupeana nafasi kwa undungu, na kwa upendeleo ila tunaweza tukaendelea tukipeana nafasi kwa uwezo, vipaji na juhudi sio kwa sababu baba yako ana hela nyingi ndio upewe hiyo Hapana" Amesisitiza Prof Mkenda


Waziri Mkenda amesema unaweza kuwa na akili nyingi lakini mvivu na mlevi, una uwezo mkubwa lakini mzembe hivyo lazima TCU isimamie ubora na kufanya kazi kwa kasi zaidi ili elimu ya Tanzania isiwe ni bora elimu bali elimu yenye ubora.


MWISHO

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com