***************
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limemshikilia RAJAB RAMADHAN[32] aliejifanya
askari polisi Kwa kutapeli watu mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dodoma Leo Julai
23,2019 Kamanda wa polisi mkoani hapa Gilles Muroto amesema kwa muda
Mrefu kijana huyo anayeishi eneo la Area A Mjini Dodoma amekuwa akijipatia
huduma mbalimbali kwa udanganyifu akijifsnya askari polisi na kutishia watu kwa
silaha bandia.
Kamanda Muroto ametaja vifaa alivyokuwa navyo mhalifu huyo kuwa ni sare ya
polisi Jangle Green,pistol ya bandia na hoster yake,picha akiwa na sare za jeshi
[JWTZ] huku uchunguzi wa awali ukionesha kuwa kijana huyo alishawahi
kuhudhuria mafunzo ya JKT na Kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu.
Katika hatua nyingine Kamanda Muroto amesema jeshi hilo limekamata vifaa vya
NIDA ambavyo ni kamera 12 ambapo mtumishi wa NIDA Ezekiel Subugo [24]
aliiba vifaa hivyo ofisini na kuwauzia watu mitaani na mtuhumiwa atafikishwa
mahakamani.
Hata hivyo,Jeshi hilo limemkamata Musa Pungu akiwa na madawa ya kulevya aina
ya Heroin kiasi cha kete 132 zilizofungashwa katika vinailoni ambapo Kamanda
Muroto amesema kijana Musa ameharibu vijana wengi kwa madawa ya kulevya
katika Mtaa wa Hazina jijini Dodoma hivyo mtuhumiwa na wenzake wanne
watafikishwa mahakamani.
Kamanda Muroto ametoa wito kwa jamii kujihadhari na Matapeli katika jiji la
Dodoma na hakuna Fedha zinazokuja kiurahisi bila kufanya kazi halali.
Sanjari na hayo,Kamanda Muroto ameipongeza Kampuni ya INNOMAX kwa
kulikabidhi jeshi hilo pikipiki mbili mpya aina ya HAOJUE na HONGLOG zenye
thamani ya zaidi ya Tsh.Milioni 4 Kwa ajili ya kufanyia doria huku akiwaasa
Watanzania wengine kuwa na uzalendo wa kusaidia jeshi hilo.
0 comments:
Post a Comment