METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, July 23, 2019

MKUTANO WA SADC NI FURSA KWA WATANZANIA-MH. BASHUNGWA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akielezea faida za maonesho ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere kuanzia Julai 5 hadi 8, 2019 ikiwa ni sehemu ya matukio yatakaofanyika kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha ujenzi wa uchumi wa viwanda unaleta matokeo chanya hapa nchini na katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)
(PICHA NA MAELEZO-DAR ES SALAAM)
*****************
NA EMMANUEL MBATILO
Wamiliki wa Viwanda hapa nchini watakiwa kujitokeza kwa wingi katika wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC itakayoanza Agosti 5 mwaka huu ili kuweza kujitengenezea ajila kupitia mkutano wa SADC.
Ameyasema hayo Leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Innocent Bashungwa katika mkutano na wanahabari.
Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam, Mh. Bashungwa amesema kuwa Tanzania imebarikiwa na rasilimali nyingi ambazo ni fursa tosha kwa Watanzania kujitengenezea ajila.
“Vijana kazi wapige kazi pasipokutegemea kuajiliwa hivyo wajikite katika kilimo na viwanda ili kujitengenezea ajila kuelekea uchumi wa Viwanda”.
Aidha Mh.Bashungwa amewataka watanzania kujivunia kwa kuwa mwenyeji wa Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC kwani kutahudhuliwa na takribani wadau 1000 katika mkutano huo.
“Tayari washiriki 580 wameshajiandikisha kushiriki maonesho hayo na matarajio yakiwa washirki zaidi ya 1000 kutoka katika nchi wanachama wa SADC na tunachoangalia kwa sasa ni namna maonesho ya wiki ya viwanda yatakavyowanufaisha Watanzania kwani hii ni fursa ya wazalishaji wetu na wamiliki wa viwanda kutangaza bidhaa zao na kupanua wigo wa masoko katika nchi wanachama“ .Alisisitiza Mh. Bashungwa.
Wiki ya viwanda itahitimishwa kwa washiriki kutembelea maeneo ya Viwanda jijini Dar es Salaam, ikiwemo eneo la ukanda maalum wa uwekezaji na kujionea utekelezaji wa shughuli za uzalishaji zinavyoendeshwa.
Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika itafanyika kuanzia Julai 5 hadi 8 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Agosti 17 na 18 Jijini humo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com