Wakandarasi wakiwa na wafadhili wa mradi wa uboreshaji huduma za maji Manispaa ya Singida eneo la Somoku |
Moja ya viongozi wa wafadhili wa mradi wa maji Manispaa ya Singida akichukua picha kwenye moja ya taki la maji eneo la Somoku. |
Muonekano wa Taki la maji eneo la Kitimo Singida likiwa limekamilika. |
Mabomba ya maji ambayo yanatumika kwenye mradi wa maji Manispaa ya Singida. |
Ukaguzi wa miradi ya maji chini ya timu ya wafadhili kutoka KFW ukiendelea mkoani Singida. |
Ukaguzi wa miradi ya maji chini ya timu ya wafadhili kutoka KFW ukiendelea mkoani Singida. |
Bi Andrea Hoeltk Mwakilishi wa KFW development Bank akibadilishana mawazo na watumishi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Mkoani Singida. |
Na Hamis Hussein - Singida
JUMLA ya wakazi takribani 500 wa Manispaa ya Singida wanatarajia kunufaika na Mradi wa Uboreshaji wa Maji unaofadhiliwa kupitia program ya IFF Woba ambapo jumla ya shilingi milioni 756 zimetengwa kufanikisha unatekelezaji uunganishaji wa huduma ya maji kwa wakazi katika maeneo ya Somoku na Mnung’una ndani ya kata ya Mungumaji.
Wakikagua
maendeleo ya mradi huo Wafadhili kutoka KFW wakiwakilishwa na Andrea Hoeltk
ambaye alisema kuwa mradi huo unaofadhiliwa kwa mkopo kutoka kwenye benki utawasaidia wananchi wa singida na pindi
utakapokamilika mamlaka ya maji mkoani hapa watapata ruzuku ya gharama za utekelezaji wake.
Akizungumza
wakati wa Ukaguzi huo Mwakilishi Kutoka Benki ya Maendeleo ya KFW Andrea Hoeltke
alisema wamefurahi Kushuhudia uwepo Mradi Huo ambao unaendelea Kutekelezwa
Chini ya Mamlaka ya Maji kupitia Ufadhili wa Benki Hiyo.
“Ni furaha kubwa kuwa Singida,
tumeshuhudia uwepo wa mradi huu unaofadhiliwa kwa mkopo wa benki, hatua hii
imeisaidia mamlaka kuwekeza kwenye miundombinu kupitia mikopo. Baada kufanikisha
mradi huu mamlaka ya maji italipata asilimia 50% ya ruzuku ,tumeona maendeleo
yake na mradi unavyowanufaisha watu wa Singida”.alisema Bi .Hoeltk
Mkandarasi
Mshauri wa Mradi Huo Grace Massawe Alisema Wameridhishwa na Utekelezaji wa
Mradi huo ambao unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Singida SUWASA Licha ya
Changamoto ambazo zilijitokeza Kabla ya Kuanza kwa Mradi Huo.
“Sisi kama wakandarasi washauri
tulianza kuuangalia mradi huu mwaka 2017 lakini kutokana na changamaoto
zilizokuwepo mbalimbali mradi ulikuja kuanza 2020, mradi huu unafadhiliwa na
KFW na sisi wakandarasi washauri tumekuwa tukifanya tathimini ya mradi, na
mpaka hapa tulipofikia tumeona unaendelea vizuri” alisema Mhandisi Massawe.
Meneja
ufundi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida mjini Suwasa
Mhandisi Richard Kasasi alisema kuwa ukaguzi unafanya na wafadhili wa mradi huo
ni sehemu ya kuangalia maendeleo yake na kuona ni jinsi gani fedha wanazotoa
zinafanya kazi.
“Hawa ndio wafadhili wa huu mradi, kwahiyo
wamekuja kuangalia katika fedha walizotoa zimefanya kazi ipasavyo, ndio maana
wamekuja kutembelea haya maeno ambayo
ukelezaji wake umefanyika katika eneo la somoku na Mnang’ana ” alisema Mhandisi Kasasi .
Mhandisi
Kasasi aliongeza kuwa mradi huo wa uboreshaji maji umetengewa shilingi milioni
756 na mradi una urefu wa mabomba ya maji Km 20.05 na umejengwa kuunganisha.
0 comments:
Post a Comment