Wednesday, May 25, 2022

WAKAZI 500 WA MANISPAA YA SINGIDA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI, SUWASA KUPATA RUZUKU


Wakandarasi wakiwa na wafadhili wa mradi wa uboreshaji huduma za maji Manispaa ya Singida eneo la Somoku

Moja ya viongozi wa wafadhili wa mradi wa maji Manispaa ya Singida akichukua picha kwenye moja ya taki la maji eneo la Somoku.

Muonekano wa Taki la maji eneo la Kitimo Singida likiwa limekamilika. 

Mabomba ya maji ambayo yanatumika kwenye mradi wa maji Manispaa ya Singida.

Ukaguzi wa miradi ya maji chini ya timu ya wafadhili kutoka KFW ukiendelea mkoani Singida.

Ukaguzi wa miradi ya maji chini ya timu ya wafadhili kutoka KFW ukiendelea mkoani Singida.

 Bi Andrea Hoeltk Mwakilishi wa KFW development Bank akibadilishana mawazo na watumishi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Mkoani Singida.


Na Hamis Hussein - Singida

JUMLA ya wakazi takribani 500 wa Manispaa ya Singida wanatarajia kunufaika na Mradi wa Uboreshaji wa Maji unaofadhiliwa kupitia program ya IFF Woba  ambapo jumla ya shilingi milioni 756 zimetengwa kufanikisha  unatekelezaji uunganishaji wa huduma ya maji kwa wakazi  katika maeneo ya Somoku na  Mnung’una ndani ya kata ya Mungumaji.

Wakikagua maendeleo ya mradi huo Wafadhili kutoka KFW wakiwakilishwa na Andrea Hoeltk ambaye alisema kuwa mradi huo unaofadhiliwa kwa mkopo kutoka kwenye benki  utawasaidia wananchi wa singida na pindi utakapokamilika mamlaka ya maji mkoani hapa watapata ruzuku  ya gharama za utekelezaji wake.

Akizungumza wakati wa Ukaguzi huo Mwakilishi Kutoka Benki ya Maendeleo ya KFW Andrea Hoeltke alisema wamefurahi Kushuhudia uwepo Mradi Huo ambao unaendelea Kutekelezwa Chini ya Mamlaka ya Maji kupitia Ufadhili wa Benki Hiyo.

“Ni furaha kubwa kuwa Singida, tumeshuhudia uwepo wa mradi huu unaofadhiliwa kwa mkopo wa benki, hatua hii imeisaidia mamlaka kuwekeza kwenye miundombinu kupitia mikopo. Baada kufanikisha mradi huu mamlaka ya maji italipata asilimia 50% ya ruzuku ,tumeona maendeleo yake na mradi unavyowanufaisha watu wa Singida”.alisema Bi .Hoeltk  

Mkandarasi Mshauri wa Mradi Huo Grace Massawe Alisema Wameridhishwa na Utekelezaji wa Mradi huo ambao unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Singida SUWASA Licha ya Changamoto ambazo zilijitokeza Kabla ya Kuanza kwa Mradi Huo.

“Sisi kama wakandarasi washauri tulianza kuuangalia mradi huu mwaka 2017 lakini kutokana na changamaoto zilizokuwepo mbalimbali mradi ulikuja kuanza 2020, mradi huu unafadhiliwa na KFW na sisi wakandarasi washauri tumekuwa tukifanya tathimini ya mradi, na mpaka hapa tulipofikia tumeona unaendelea vizuri” alisema Mhandisi Massawe.

Meneja ufundi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida mjini Suwasa Mhandisi Richard Kasasi alisema kuwa ukaguzi unafanya na wafadhili wa mradi huo ni sehemu ya kuangalia maendeleo yake na kuona ni jinsi gani fedha wanazotoa zinafanya kazi.

“Hawa ndio wafadhili wa huu mradi, kwahiyo wamekuja kuangalia katika fedha walizotoa zimefanya kazi ipasavyo, ndio maana wamekuja kutembelea haya maeno  ambayo ukelezaji wake umefanyika katika eneo la somoku na Mnang’ana ” alisema Mhandisi Kasasi .

Mhandisi Kasasi aliongeza kuwa mradi huo wa uboreshaji maji umetengewa shilingi milioni 756 na mradi una urefu wa mabomba ya maji Km 20.05 na umejengwa kuunganisha.

 

 

 


No comments:

Post a Comment