METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 5, 2022

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan afungua Mkutano wa Maridhiano ya Kitaifa, Haki na Amani Jijini Dodoma

         

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa, Mabalozi, Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali kabla ya kufungua Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma.

   

Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa, baadhi ya Mabalozi wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma kuhudhuria Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano, ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara) Abdulrahman Kinana katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama vya Siasa waliohudhuria Mkutano wa Amani, Haki na Maridhiano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,  Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara) Abdulrahman Kinana wakitoka nje ya ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma baada ya kuzungumza na viongozi mbalimbali wa vyama vya Siasa waliohudhuria Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara) Abdulrahman Kinana nje ya ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma baada ya kuzungumza na viongozi mbalimbali wa vyama vya Siasa waliohudhuria Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com