Na HAMIS HUSSEIN, Singida
CHAMA cha Girl Guides Tanzania (TGGA) kimedhamiria kutoa mafunzo kwa walimu kutoka shule za Sekondari na Msingi kutoka Halmashauri za wilaya ya Ikungi, Singida DC na Manispa mkoani Singida yaliyowalenga wasichanaa na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumzia mafunzo hayo Afisa Mradi Msaidizi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabia nchi na Mazingira kutoka TGGA, Praxeda Swai alisema mafunzo hayo ya siku nne yamewalenga walimu hao na wasichana ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na masuala ya tabia nchi na kugombea uongozi.
“Baada ya kuwapatia mafunzo haya walimu na wanajamii ambao tumewakutani hapa wataenda kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kuchukua hatua chanya cha kukabiliana na changamoto za tabia nchi 'mfano Mkoa wa Singida ambao umekuwa ukikabiliwa na ukame na ukiaangalia ukame huyu unatokana na ukataji wa miti',hivyo mafunzo hayo wataweza kupambana na mabadiliko ya tabianchi” alisema Swai.
Alisema kazi kubwa watakayokuwa wasichana na watoto wakike ni kuihamasisha jamii kupanda miti kwani wahanga wakubwa kunapokuwa na ukame ni wasichana na mama zao ambao wanakuwa wakiangaika kwenda kutafuta maji wakitumia muda mwingi na umbali mrefu na kuwa lengo lao ni kuifanya Singida kuwa ya kijani.
Utangulizi wa Mafunzo hayo umelianza leo katika Ukumbi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Singida ambapo mafunzo ramsi yatafunguliwa kesho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini Mhandisi Paskas Muragili na yanatarajiwa kufikia tamati Aprili 10, 2022.
0 comments:
Post a Comment