Angela Msimbira -TAMISEMI
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kasimu Majaliwa ameiagiza
Ofisi ya Rais- TAMISEMI kupitia Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanatekeleza
Mpango wa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri zao.
Akizundua
Mipango ya kuendeleza sekta ya Kilimo ya Wilaya uliofanyika katika ukumbi wa
Mikutano wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma leo tarehe 2 Machi, 2022 Mhe.
Majaliwa amesema utengaji wa maeneo ni kuhimu ili kila mwekezaji anapohitaji
eneo ka kuwekeza apate kwa haraka bila urasimu.
Mhe.
Majaliwa ameelekeza kuwataka Wakurugenzi
kutenga maeneo ya uwekezaji ili kuwawezesha wananchi kufanya kazi zao za
kilimo, ufugaji na ujenzi wa viwanda katika mazingira bora na yanayotambulika.
Amesema
yapo maeneo ambayo ni makubwa lakini bado yanamilikiwa na watu, Serikali
imeshafanya mapitio ya kuyatambua maeneo hayo, hivyo ameziagiza Halmashauri
zote nchini kuhakikisha wanasimamia maeneo.
‘Maafisa ugani wasimamiwe kimalifu na
wawezeshee vitendea kazi kama usafiri nk kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao’
Mhe Majaliwa Amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanawapangia kazi maafisa ugani kulingana na fani walizosomea ili kuleta tija na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao kulingana na Jiografia ya maeneo yao.
Akiwa
katika Mkutano huo Mhe. Majaliwa ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha
wanatenga fedha kutoka katika mapato ya ndani
ili kutekeleza mpango wa maendeleo ya kilimo , mifugo na uvuvi wa Wilaya na fedha hizo zitoke kwenye tozo za maeneo
hayo ili kutumika kuendeleza mpango huo.
Katika hatua nyingine amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanaongeza usimamizi wa fedha na rasilimali zilizopo kwa kujenga uwezo wa kusimamia utekelezaji wa miradi katika ngazi zilizopo na kubuni vyanzo vingine vya kupata fedha ili kuendeleza miradi ya kilimo katika maeneo yao
Naye,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuziagiza Halmashauri zote nchini kuleta taarifa ya maeneo ambayo wametenga kwa ajili ya uwekezaji.
0 comments:
Post a Comment