METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 17, 2021

RC MWANZA AKABIDHIWA MADARASA 97 NI YALE YALIYOJENGWA KWA FEDHA ZA MPANGO WA MAENDELEO KWA USTAWI NA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO 19







Na Maganga James Gwensaga – Mwanza 

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza imekabidhi vyumba 97 vya madarasa kwa Mkuu wa mkoa huo mhandisi Robert Gabriel vilivyojengwa kwa fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya uviko 19

Akikabidhi vyumba hivyo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Disemba 16, 2021 shule ya Sekondari Bujinga Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Apolinary alisema walipokea kiasi cha shilingi 1,940,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 97 na seti ya meza na viti 4,850 ikiwa ni fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya uviko 19 lengo likiwa ni mpango wa serikali kuhakikisha miundombinu ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2022 inakidhi mahitaji.

“ Lengo la pili Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ni kuendelea kukidhi mahitaji ya udahili ambapo tumejenga shule mpya tatu zenye jumla ya vyumba vya madarasa 16 na hivyo kufanya halmashauri kuwa na ziada ya vyumba vya madarasa 16.”Alisema Mkurugenzi

Aidha alibainisha kuwa mahitaji kwa mwaka wa masomo 2022 ilikuwa ni vyumba vya madarasa 211 kwa ajili  ya wanafunzi 10662(was 5436 na wav 5226) huku vyumba vilivyopo ni 114 na upungufu ni madarasa 97 hivyo wanaishukuru sana serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwapatia fedha hizo za ujenzi na kukamilisha ujenzi wa vyumba 97 vitakavyokidhi mahitaji ya wanafunzi wote waliofaulu na watakaojiunga na kidato cha Kwanza mwaka 2022. 

Akizungumzia mafanikio ya ujenzi wa vyumba hivyo alisema mbali na kusaidia wanafunzi wote waliochaguliwa kidato cha kwanza mwaka 2022 kujiunga na kidato cha kwanza pia jamii imepata utambuzi namna ya kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao na uwepo wa ofisi ya walimu  umesaidia kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vyumba hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mhandisi Robert Gabriel aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuwa mfano kwa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati akiitaja kuwa Halmashauri ya kufanyiwa  mfano kwa Halmashauri nyingine nchini.

“ Nianze kwa pongezi kwa Mkuu wa wilaya kwa usimamizi mzuri wa kizalendo wa maagizo ya kimamlaka ndani ya Halmashauri na wilaya ya ilemela, lakini pia niwapongeze wajumbe wa kamati ya usalama ya  wilaya lakini, mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi pia kwa kusimamia miradi hii bila kumsahau Mbunge wa Ilemela kwa usimamizi wa fedha pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kazi kubwa iliyofanyika.” Alisema Mhandisi Gabriel 

“ Kubwa Zaidi nimpongeze sana kiongozi Mkuu wa Taifa letu la Tanzania Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizoleta mapinduzi makubwa sana kwenye Mkoa wetu na hasa Ilemela, haya ni mapinduzi makubwa sana.” Aliongeza kusema 

Alisema Ilemela imekuwa ikifanya vizuri katika mambo mengi hata kwenye kampeni ya chanjo ilikuwa mstari wa mbele hivyo imekuwa wilaya ya mfano kwa wilaya nyingi nchini. 

Aidha alisema Ilemela wameonyesha uzalendo mkubwa sana kwenye suala la matumizi ya fedha kwani baadhi ya viongozi zikiletwa fedha hufikiria kuziweka mifukoni lakini hali ni tofauti kwa Ilemela fedha zimetumika vizuri na kwa uaminifu mkubwa na huo ndo uzalendo wenyewe.

“ Niwaombe sana wananchi na viongozi wa Ilemela tuendelee kuwa wazalendo kwenye kila fedha ya umma inapokuja muisimamie kikamilifu kwa namna hiyo tutapiga hatua kubwa sana ya maendeleo.” Alisema Mkuu wa Mkoa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala alimshukuru Mheshimiwa Rais  kwa kazi kubwa anayoendela kuifanya tangia aingie madarakani kwa jitihada kubwa anazoendelea kuzifanya akijibu kwa vitendo chngamaoto zilizokuwa zikiwakabili wananchi,

“ Hiki tunachokifanya leo ni sehemu ndogo ya kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita kwni  iko miradi mingi ambayo Mheshimiwa Rais amekuwa akiitolewa fedha ikiwemo miradi ya maji, barabara, umeme , afya lakini pia kwenye elimu kwa sehemu kubwa sana amekua akitoa fedha na kwa niaba ya wana ilemela tunashukuru sana.” Alisema Masala 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com