Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge (wa kwanza kulia ) akiongea na
wafanyabiashara hivi karibuni katika
soko la kilambida Kata ya Kindai
manispaa ya Singida ikiwa ni ziara yake ya kuangalia hali ya mazingira
ya usafi na miundombinu mbalimbali ya masoko.
Kaimu
Mkurugenzi manispaa ya singida Dk. Adrianus Kalekizi( wa kwanza kulia
) akitoa ufafanuzi katika baadhi ya hoja zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa katika
ziara yake ya hivi karibuni katika masoko ya manispaa hiyo.)
Na
Bashiri Salum -Singida
MKUU
wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge leo Machi 2, 2022 ametembelea masoko ya Kilambida,
Mitunduruni na Mahembe yaliyopo katika Manispaa
hiyo lengo likiwa ni kukagua mazingira ya usafi pamoja na maeneo
waliyokwisha pangiwa kufanyia biashara ya mazao ya chakula.
Akiwa
katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa huyo alimuagiza Mkurungezi wa Manispaa ya
Singida kutafuta fedha kwa ajili ya kulipa
fidia kwa wamiliki wa makaburi yaliyopo soko la mahembe ili kupisha
wafanyabiashara pamoja na kufanya
marekebisho ya miundombinu katika baadhi
ya maeneo hayo.
Dk.
Mahenge alisisitiza juu ya ujenzi wa
maegesho ya magari na sehemu za kushushia mizigo pamoja na kulifanya soko la
Mahembe kama sehemu ya kushushia ndizi na viazi kutokana na maeneo mengine kuwa
yameshajaa
Hata
hivyo Dk. Mahenge aliitaka Manispaa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa ya
kila kinachoendelea kuhusu fidia za
makaburi na baadhi ya wamiliki wa nyumba ambazo zinatakiwa kupisha eneo la soko
na kuwataka kuweka utaratibu ambao hautachelewesha utekelezaji wa shughuli
hizo.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akawataka
wafanyabiashara hao kuhakikisha kwamba wanabaki katika maeneo yao waliyopangiwa
wakati serikali ikiendelea kupambana na changamoto zinazojitokeza.
Mhandisi
Muragili aliwataka viongozi wa masoko
kuelimishana ili kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali
ya masoko ikiwa ni pamoja na kukubali kufanya maendeleo wakati taratibu za
malipo ya fidia yakiendelea.
Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Dk. Adrianus Kalekizi amemueleza Mkuu wa Mkoa
kwamba Manispaa imejipanga kuhakikisha zoezi
litakamilika ifikapo mwezi Mei 2022 ambapo kwa sasa tayari bajeti yake imeshapangwa.
Ziara
hiyo ya Mkuu wa Mkoa iliwahusisha Viongozi wote wa Manispaa kamati ya ulinzi na
usalama pamoja na wataalamu mbalimbali wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment