Taasisi ya Aga khan nchini kupitia mradi Mtambuka wa Saratani (TCCP) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) imeendesha mafunzo ya siku moja kwa waandishi wahabari Mkoani Mwanza kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kuandika habari zinazohusu Saratani.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini humo
March 25, 2022 yakihusisha waandishi Zaidi ya 30 kutoka vyombo mbalimbali, Dkt
Beda Likonda Daktari Bingwa wa Matibabu ya Saratani alisema kwa mwaka Tanzania
inapata wagonjwa wapya 40,000 wa matatizo ya saratani huku asilimia 10 ya wagonjwa hao
ni saratani ya shingo ya kizazi, matiti, tezi dume na saratani nyinginezo. .
“ Kutokana na ukubwa wa tatizo hili tumeona sasa
tuje kwa pamoja kuangalia namna ya kupambana na tatizo hili, hivyo
tunawashukuru sana wenzetu wa taasisi ya Aga khan kupitia mradi wao wa TCCP
kuona kwamba iko haja ya kusimama pamoja
kutoa elimu na kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kushughulikia tatizo hili”
Alisema Dkt Beda
Alisema Changamoto ambazo wanazipata katika hii tiba maana yake wale wanaowaangalia wanaopambana
na ugonjwa huo yaani nchi za magahraibi
kuna mihimili mikubwa minne ambayo wakiitendea haki wanaweza kupata matokeo mazuri.
Aliutaja Muhimili wa kwanza kuwa ni takwimu kwani
takwimu za kwanza ni makisio, wa pili ni kinga ambapo wanatakiwa kutoa elimu kuhusu kansa ni nini,
chanzo chake, inatokana na nini,
tunajizuiaje nk na mhimili wa tatu ni tiba ambapo serikali inatakiwa
kuhakikisha kuanzia katika hatua
mbalimbali za vituo vya tiba kama zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya
na mkoa kuwepo na huduma za
kuwafikia wananchi.
“ Na mhimili wanne ni tiba shufaa pale mgonjwa
anaporudi nyumbani na hakuna uwezo wa kumtibu
basi hata ikitokea amefariki,
afariki awe hana matatizo mengi yaani ubora wa afya yake ushughulikiwe .” Aliongeza Dkt Beda
Alisema katika mihimili minne kuna mapungufu mengi
wamefurahi watu wa Aga Khan wakishirikiana na wafaransa kuungana ili kuona wanaifikiaje
hii mihimili yote minne na watakuwa wameanza na mihimili miwili wakiamini
baadae wanaweza kuikamilisha mingine miwili ili waweze kupigana vizuri na adui
Saratani(Kansa).
Akitoa mafunzo hayo kwa waandishi Dkt Athanas
Ngambakubi Daktari Bingwa wa upasuaji kutoka hospitali ya Mkoa Sekouture
alisema katika Tanzania saratani ya Shingo ya kizazi kwa wanawake ndiyo
inayoongoza ambapo kwa mwaka 2020 yaliripotiwa maambukizi mapya 10,241 ambayo
ni sawa na asilimia 25.3 na vifo asilimia 24.2
Alizitaja dalili zake kuwa ni kutoka damu ukeni
isivyo kawaida na tofauti na hedhi, kupata hedhi yenye damu nyingi na maumivu
Zaidi ya kawaida na maumivu, kutoka damu ukeni wakati au baada ya kujamiiana na
mwenza na pia kutoka majimaji ukeni isivyo kawaida na yenye harufu mbaya.
Dalili zingine ni maumivu ya kiuno, nyonga na mgongo
pamoja kuchoka mara kwa mara.
Alisema uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ni
kumwangalia mama kwa kutumia kifaa kiitwacho speculum lakini kwa wenye umri
Zaidi ya miaka 30 lakini kwa wenye umri chini ya huo hawazuiliwi kwenda
kufanyiwa uchunguzi.
Aidha alisema Serikali imeendelea kuchukua tahadhari
mbalimbali dhidi ya ugonjwa huo ikiwemo chanjo iliyotolewa kwa mabinti kuanzia
miaka 9 lakini pia namna ya kujikinga ikiwemo kuepuka ngono katika umri mdogo.
“ Licha ya kuwa saratani ni hatari tunaweza kuepuka
maambukizi kwa kuepuka ngono katika umri mdogo, kuwa na mwenza mmoja mwaminifu,
kutumia kondomu wakati wa kujamiiana, kula mbogamboga na matunda kwa wingi
pamoja na kuacha matumizi ya tumbaku na kupunguza matumizi ya Pombe.” Alisema
Dkt Athanas
Nao waandishi waliohudhuria mafunzo hayo
waliishukuru sana taasisi ya Aga Khan kwa kuwapa mafunzo hayo kwani
yatawaongezea ufahamu Zaidi katika kuandika habari zinazohusu ugonjwa wa
saratani.
Mmoja wa waandishi hao Alphonce Tonny kutoka Yuhoma
tv alisema alikuwa akiifahamu Saratani lakini hakujua kama kuna aina mbalimbali za
Saratani na matibabu yake.
“ Ukweli nilikuwa najua kuna Saratani lakini nilikuwa sijui kama kuna aina mbalimbali, uchunguzi wake, sababu
zake na tiba zake kupitia mafunzo haya naamini uandishi wangu utabadilika sana
na sasa jamii itafahamu kwa undani Zaidi na kwa kina kuhusu ugonjwa huu na mimi
kama mwandishi ntatumia taaluma yangu kuondoa Imani potofu iliyojengeka kwa jamii
na hata ofu juu ya ugonjwa huu kwamba ukiupata hauwezi kupona kumbe kuna watu
wanaugua na kupona.” Alisema Alphonce
Mradi Mtambuka wa Saratani wenye thamani ya Euro
13.3 unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa(AFD) na Aga Khan Foundation(AKF) una lengo la
kuboresha miundombinu na vifaa tiba vya huduma ya saratani, kuendeleza na
kukuza rasilimali watu wa taaluma mbalimbali za matibabu ya saratani, kuboresha
huduma na uhamasishaji wa saratani katika jamii na kudumisha ushirikiano na
tafiti kuhusu saratani nchini.
Aidha utatekelezwa katika wilaya 13 za Mikoa ya
Mwanza na Dar es salaam katika kipindi cha miaka minne ambapo kwa kushirikiana
na timu za mikoa hiyo itaboresha huduma za awali za saratani katika vituo 100 (
50 Dar es salaam / 50 Mwanza ) vya afya, huku manufaa yake yakitajwa kuenea
nchi nzima.
Baadhi ya mafanikio hayo ni kufungwa kwa mashine ya kisasa ya Ultrasound katika taasisi ya Ocean Road yenye thamani ya Tzs 150 milioni ambayo inahudumia takribani wagonjwa 50-80 kwa siku, uwepo wa mashine ya kisasa ya uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti(3D Mammography Machine) yenye thamani ya Tzs 800 milioni ambayo inahudumia wagonjwa takribani 20-25 kwa siku.
0 comments:
Post a Comment