METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 2, 2022

Waumini wachangishana Mil 270 ujenzi wa kanisa//WAZIRI MKENDA Aongoza Harambee

Waumini wa kanisa Katoliki, Parokia ya Tarakea wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro wamechangishana zaidi ya Sh 270 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kanisa katika kigango cha Nanjara ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiroho.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa kanisa hilo katika Harambee iliyofanyika katika kigango hicho mbele ya Mbunge wa Rombo na Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda, Katibu wa Kigango hicho Adolf Mushi amesema waumini wa kanisa hilo wameonyesha unyoofu wa moyo.

Amesema mpaka sasa ujenzi wa kanisa hilo umefikia zaidi ya asilimia 70 ambapo waumini ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za kiroho wataondokana na adha hiyo siku za hivi karibuni.

"Mpaka sasa wananchi na waumini wa kanisa hili wamejichangisha fedha zaidi ya Sh270 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hili na mpaka sasa lipo hatua za mwisho kukamilika," amesema.

Hata hivyo, Profesa Mkenda aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya ujenzi wa kanisa hilo, amesema wananchi wa Rombo wamekuwa ni mfano wa kuigwa katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuitaka jamii kuendelea kuwa na moyo huo huo.

"Ninashukuru sana wananchi wangu wa Rombo mmekuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo, sio tuu za serikali bali hata hizi za kanisa mmekuwa mstari wa mbele.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com