Waziri wa ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Inocent Bashungwa akizungumza na wakuu wa mikoa kuhusu mifumo ya anwani ya makazi hafla iliyofanyika Jijini Dodoma
Baadhi ya Wakuu wa mikoa wakifuatilia kikao kazi kuhusu mfumo wa anwani ya makazi
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na washiriki wa kikao cha Wakuu wa mikoa Jijini Dodoma
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango na Waziri Mkuu Mhe. Kasimu Majaliwa wakimuonyesha bango ilipo ofisi ya Rais Ikulu ya Chamwino Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan , kwa pamoja wakifurahia kwenye kikao na wakuu wa Mikoa Jijini Dodoma jana.
Jopo la viongozi Meza kuu katika kikao na Wakuu wa Mikoa kuhusu Mifumo ya Anwani ya Makazi Kilichofanyika Jijini Dodoma
Na Mathias Canal - Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewataka Viongozi kuhakikisha
wanafuatilia na kusimamia kikamilifu matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi ili
kusaidia upatikanaji wa huduma kirahisi kwa wananchi.
Mhe.
Bashungwa amesema hayo leo Jijini Dodoma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
kwenye kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu mfumo wa anwani za
makazi amesema, Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeshirikiana na Wizara ya Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
kutoa maelekezo kwa Sekretarieti
za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa utekelezaji wa anwani za makazi.
Amesema
kwa majukumu yaliyotekelezwa na Wizara
kwa kushirikiana na wadau kuhusu anunwani za makazi ni pamoja na
kuandaa miongozo ya mfumo wa anwani za makazi, kutunga sheria ndogo, utambuzi
wa majina ya mitaa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 184 Nchi nzima, kuandaa
ramani za mipaka ya kiutawala, kujumuisha masuala ya mfumo wa anwani za makazi
kwenye mwongozo wa mpango na bajeti katika mfumo wa undaaji wa bajeti.
Mhe.
Bashungwa amemuhakikishia Mhe. Rais Samia
Ofisi ya Rais, TAMISEMI itaendelea
kuratibu na kusimamia anunwani za makazi zinatekelezwa katika Mamlaka za
Serikali za Mitaa na wadau ifikapo Mei,2022 kama ilivyoainishwa katika mpango
husika na uandaaaji wa ramani msingi na kuanzia ngazi ya kitongoji, mtaa,
kata mpaka Mkoa.
Amezielekeza
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinahakikisha
zinashirikiana na wadau kuandaa majina
ya barabara na mitaa na kuziwasilisha Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari.
“Ninazielekeza Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhamasisha wananchi na wadau washiriki katika usimakaji wa nguzo
za majina ya barabara na mitaa,
kubandika vibao vyenye namba za nyumba
na mitaa” alisema Mhe. Bashungwa
Aidha,
alisema utoaji wa elimu kwa viongozi, watendaji na wananchi kuhusu utekelezaji
na matumizi ya mfumo wa anwani za makazi
unazingatiwa na amemshukuru Mhe.
Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza maendeleo kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment