METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, January 3, 2022

MBUNGE MTATURU AISHUKURU SERIKALI HATUA ZA UPATIKANAJI MAJI JIMBO LA IKUNGI






Timu ya Wataalam wa Maji kutoka Bonde la Maji kanda ya kati kituo cha Singida wakiongozwa na Ndugu Mushuro wameendelea na kazi ya utafiti kwenye kijiji Cha Damankia ili kujua ubora na wingi wa maji maeneo hayo hatimae mitambo ya kuchimba visima virefu iweze kufika  kwa ajili ya kuwapatia wananchi maji safi na salama kwenye jimbo la Singida Mashariki. 

Kazi itafanyika kwa wiki hii nzima kuanzia tarehe 3 Januari 2022 kwenye vijiji vya Msule, Mampando, Ujaire, Mang'onyi na Mbwanjiki. 

Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu akiongea na mwandishi wetu amemshukuru sana mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutimiza dhamira yake ya kuwapatia wananchi maji safi na salama. 

#SingidaMashariki#MaendeleoKipaumbeleChetu#
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com