METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 8, 2020

NAIBU WAZIRI DKT ANGELINE MABULA AMTEMBELEA MJANE WA BABA WA TAIFA BUTIAMA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza mjane wa Baba wa Taifa Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere Bi Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Butiama mkoa wa Mara jana wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiagana na  mjane wa Baba wa Taifa Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere Bi Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Butiama mkoa  wa Mara jana wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati ya Ardhi Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Mwl Nyerere Profesa Agnes Mwakaje alipokuwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoa wa Mara jana.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemtembelea Mjane wa Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Butiama mkoa wa Mara.

Dkt Mabula alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani Butiama kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi sambamba na kugawa hati za ardhi kwa wananchi wa Butiama mkoani Mara waliopimiwa na kumilikishwa maeneo yao.

Naibu Waziri mbali na kutembelea wilaya ya Butiama pia alitembelea wilaya za Musoma, Rorya na Tarime ambako alizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi, alikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi na kufuatilia maelekezo aliyoyatoa kuhusiana na masuala ya ardhi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com