Kwaya ya Gosipo ya kanisa la Pentekoste (FPCT) Singida mjini kati,ikitumbuza kwenye ibada ya kwanza ya mwaka huu (2022).
NA NATHANIEL LIMU - SINGIDA
WAUMINI na
wasio waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Singida,wameshauriwa
kutenga muda kwa ajili ya kumshukru Mungu kwa kitendo chake cha kuwavusha
salama mwaka jana (2021),ambao uligumbikwa na changamoto nyingi ngumu
kupitiliza,ikiwemo kuondokewa ghafla na kipenzi cha wanyonge Hayati Dk. John Magufuli
na Aliyekuwa rais wa awamu ya tano .
Wito
huo umetolewa askofu mstaafu wa kanisa la Pentekoste (FPCT) Singida mjini
kati,Dk.Paulo Samweli,wakati akizungumza muda mfupi kabla ya mahubiri maalum ya
kuaga mwaka 2021 na kukaribisha mwaka mpya wa 2022,kufanyika.
DK.Samweli
alisema sio Tanzania pekee iliyopita katika kipindi kigumu mwaka jana,ni karibu
dunia nzima zikiwemo nchi zilizoendelea katika nyaja zote.
Amefafanua
kwamba mapema mwaka jana, wakati nchi mbalimbali duniani ikiwemo zilizoendelea
kama Marekani kujifungia ndani ya nyumba kukwepa corona,Watanzania waliendelea
kuchapa kazi halali.Pia walihudhuria nyumba za ibada bila masharti yo yote.
Aidha,askofu
huyo mstaafu,alisema kitendo cha kuondokewa ghafla na Hayati Dk.Magufuli sio
tukio la kitoto,ni tukio ngumu mno.Watanzania walitaraji katika awamu yake ya
mwisho,angeenda kuiletea nchi maendeleo ambayo yageishangaza dunia.
“Kwa ujumla sisi sote
bila kujali itikadi zetu za dini na kisiasa, tunawajibika kufanya ibada kwa
ajili ya kumshukuru Mungu kutuvusha salama mwaka jana. Vilevile tuombe mwaka
huu tuliouanza juzi uwe wa amani na utulivu mkubwa.”,alisema
askofu Dk samweli.
Awali
mwinjilisti wa kanisa hilo,Ernest Samsoni,alisema mwaka mpya wowote ule,
unatawaliwa na mabadiliko mapya ya kila aina.
“Mwaka mpya unakuwa na
namba mpya,umri wa mtu tarakimu za namba zinabadilika, mambo ya mtu
binafsi yanabadilika, kifamilia na hata Taifa kuna kuwa na mabadiliko mengi ili
kuendana na wakati. Kupitia mabadiliko hayo mhusika kwa vyo vyote,atapiga
hatua kiuchumi na kijamii” alisema.
Pia mwinjilsti
huyo, amezitaka kwaya mbalimbali za kanisa hilo kutanua wingo zaidi wa nyimbo
zao, ili ziwafikie watu wengi zaidi.
“Nyimbo zenu kama
zitaendelea kusikika tu ndani ya kanisa letu, kitendo hicho kitakuwa kama
mnajichimbia ndani ya box.Kuwenu wabunifu na hakikisheni kazi yetu inajulikana
ndani na nje ya mkoa wa Singida na ikiwezekana nje ya nchi”,alisema
Mwinjilsti Ernest kuzishauri kwaya hizo.
Katika
ibada ya kwanza kwa mwaka huu iliyofanyika 02/01/2022 Askofu Dk.Samweli,alisema
katika mwaka ulioanza juzi,kanisa litatekeleza maagizo yaliyopo
kwenye kitabu kitakatifu cha Tito 03 mstari mdogo wa 14 unaosema ‘Watu wetu nao wajifunze kudumu katika
matendo mema,kwa matumizi yaliyo lazima,ili wasiwe hawana matunda’.
Akifafanua,alisema
kila muumini wa kanisa hilo analo jukumu la kuhakikisha kanisa linasonga mbele
kwa matendo mema,ili makanisa mengine yakimbilie kujifunza uendeshaji bora wa
kanisa.
“Kanisa lazima liwe na
mabadiliko yenye tija zaidi.Tuwe wabunifu tutembelee nyumba zingine za ibada
ili kujifunza kutoka makanisa mengine.Tukijifunza yale mazuri na yanayompendeza
Mungu,kanisa letu litasogea mbele.Lakini tusipojifunza,kanisa
litadumaa na halitakuwa na mambo mapya”,amesisitiza Dk.Samweli.
0 comments:
Post a Comment