METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 2, 2021

WAKULIMA ARUSHA WAPEWA ELIMU YA USAJILIWA VYAMA VYA UMWAGILIAJI NA UCHANGIAJI WA ADA NA TOZO

Kaimu Mkurugenzi wa Mipango toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Reginald Diyamet na Mhandisi Naomi Mcharo, wakijadili jambo linalohusu Kilimo cha Umwagiliaji kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020.

Bi. Fatuma Mwera,Afisa Kilimo toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akiongea na viongozi wa skimu za umwagiliaji katika wilaya ya Arusha kuhusiana na maswala ya Tozo na Ada za umwagiliaji.

  Na; Mwandishiwetu – Arusha

Wakulima katika skimu zakilimo cha umwagiliaji Mkoani Arusha, wamepewa elimu kuhusiana na namna ya kusajili vyama vya umwagiliaji na utoaji wa ada na tozo na kupewa utaratibu w a kulipia ada hizo zitakazosaidia kuboresha na kurekebisha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji pale itakapokumbwa na madhara yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia nchi au uchakavu. 

Bi Fatuma Mwera Afisa Kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumza na baadhi ya viongozi wa skimu za kilimo cha umwagiliaji katika Halmashauri ya Arusha katika kata ya Ilikiding’a alibainisha kuwa, usajili wa vyama vya umwagiliaji utasaidia skimu kutambulika na kupata fursa zinazojitokeza ikiwa ni pamoja na kupelekewa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.

Aidha aliwaasa viongozi hao kuwa vinara katika swala zima la usimamizi na utunzaji wa mazingira hususani vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kutokufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo hivyo. 

Aliendelea  kusemakuwa,skimu zote za kilimo cha umwagiliaji zitafanyiwa maboresho kwa awamu lakini ,skimu ambazo zimesajiliwa ndizo zitakazopewa kipaumbele kwanza wakati wa maboreshohayo. 

“ Ni vizuri kusajili wote kwa pamoja ili tupange mipango ya kazi kirahisi na kuzifikia skimu kwa awamu, Alisisitiza.”

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com