METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, December 15, 2021

TANZANIA NA MAREKANI ZAENDELEA KUSHIRIKIANA SEKTA AFYA IKIWEMO MAPAMBANO YA UVIKO -19

 






SERIKALI ya Tanzania na Marekani kupitia Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa (CDC) zimeendelea kufanya majadiliano ya masuala mbalimbali katika Sekta ya Afya ikiwemo kujadili mwenendo wa UVIKO - 19. 

Kupitia Kikao cha majadiliano kilichofanyika  15 Desemba 2021 katika ofisi za Wizara ya Afya jengo la Bima ya Afya NHIF jijini Dodoma ambapo Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima amekutana na kufamya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa CDC hapa nchini Bw. Mahesh Swaminathan.

Dkt Gwajima ameeleza hatua zilizofikiwa katika kukabiliana na UVIKO - 19 ambapo takwimu zinaonyesha hadi kufikia tarehe 13 Desemba 2021 watu 1,228,760 wamepata chanjo ya ugonjwa huo. 

Amesema kuwa ili kuongeza kasi ya chanjo hapa nchini kwa lengo la kufikia lengo la kutoa chanjo kwa hiyari kwa asilimia 60 ya Watanzania, Serikali imejipanga kufanya kikao kazi cha majadiliano na wakuu wa mikoa wote Tanzania Bara kitakachofanyika jijini Arusha tarehe 22 Desemba 2021.

 Lengo la kikao hicho  ilikuwa ni kujadili vipaumbele vitakavyowezesha kufikia malengo ya uchanjaji katika Mikoa na Halmashauri zote hapa nchini. 

" Serikali imejiwekea mikakati ya kuongeza kasi ys uchanjaji ambapo huduma za chanjo zitajumuishwa kwenye kliniki za magonjwa na huduma zinazotolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya". Alisema Dkt. Gwajima. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa CDC,  Mahesh ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa Shirika hilo litaendelea kudumisha uhusiano uliopo kwa lengo la kuhakikisha usalama wa Afya za wananchi huku akimpongeza Waziri wa Afya Dkt Gwajima kwa kusimamia kikamilifu Zoezi la kukabiliana na maambukizi ya UVIKO - 19

Aidha, Mahesh amesema kuwa shirika la CDC limeweka kipaumbele cha kushirikiana na serikali katika kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa washukiwa wa magonjwa ya milipuko ikiwemo UVIKO. Vilevile, shirika hilo litaendelea kutoa msaada katika huduma za uchunguzi wa maabara na pia kuchangia kwenye jitihada za Serikali katika kuongeza kasi ya uchanjaji.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com