Na Maelezo-Zanzibar
Chama cha
Wakulima (AFP) kimelaani vikali dhidi ya hujuma zilizoandaliwa kufaywa
na Umoja wa Wananchi UKAWA ifikapo tarehe 1mwezi ujao.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Chama hicho Said Soud Said katika
Ukumbi wa Sanaa uliopo Rahaleo Zanzibar amesema hujma hizo
zilizoandaliwa na UKAWA za kufanya maandamano makubwa ya kupinga
Serikali iliopo madarakani zilizopangwa nchi nzima zina lengo la
kuvuruga amani nchini.
Amesema
Jeshi la Polisi na Wananchi kwa ujumla wametakiwa kuwa macho kutokana na
kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa siasa za kutaka kuchafua
kwa makusudi na kuipeleka nchi katika vurugu jambo ambalo litasababisha
kuwepo vitendo vibaya ikiwemo ubakaji na mauaji.
Aidha
amesema Zanzibar haiwezi kuvumilia kuingia katika vurugu hivyo Wananchi
wasikubali kushawishiwa na Wanasiasa wasiopenda maendeleo wanaotaka
kuvuruga amani iliopo.
“Vijana
msikubali kushawishiwa na Wanasiasa wamejitokeza kwa ajili ya biashara
hivyo natoa indhari hii kwa kuwatahadharisha wazanzibari wenzangu
kuachana na hujuma hiyo inayoandaliwa,”Alisema Said Soud.
Hata
hivyo amewaasa Vijana kutokubali kushawishiwa na Wanasiasa kushiriki
katika vurugu na badala yake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
shughuli za kiuchumi na maendeleo kwa lengo la kujikimu kimaisha.
Akizungumzia
suala la amani na utulivu Pemba Mwenyekiti huyo amefahamisha kuwa hali
sasa ni yakuridhisha kutokana na kupungua kwa kasi vitendo vya
hujumaVisiwani humo na.
“Jeshi la
polisi kwa kushirikiana na Serikali wamesaidia kwa kiasi kikubwa na
kuwadhibiti wale wote walioshiriki kufanya vitendo hivyo kwa kuchukuliwa
hatua za kisheria,” ameeleza Mwenyekiti huyo .
0 comments:
Post a Comment