Serikali
ya Sudan Kusini imewaajiri watoto wavulana kama wanajeshi wakati huu
inapojiandaa kwa mzozo mpya, kwa mujibu wa shirika la Associated Press.
Mwanasiasa
mmoja mwenye ushawishi anaripotiwa kuongoza shughuli ya kuwaajiri
watoto hao, wengine wakitajwa kuwa na umri wa hadi miaka 12 kutoka
kijiji kimoja nchini humo.
Nyaraka
zinaonyesha kuwa shughuli ya kuwaajiri watoto hao, ilifanyika muda mfupi
baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuidhinisha azimio wiki
moja iliyopita la kutuma wanajeshi 4000 kwenda Sudan Kusini, kuwalinda
raia baada ya kuzuka mapigano mapya katika mji mkuu Juba mwezi uliopita.
Mapigano
hayo yamekuwa kati ya vikosi watiifu kwa rais Salva Kiir na vile vya
makamu wake aliyefutwa kazi Riek Machar ambaye tayari ameikimbia nchi
hiyo.
Zaidi ya watu 100,000 walikimbia makwao baada ya mapigano ya mwezi Julai
Shirika
la kuwahudumia watoto la umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya
watoto 650 wameajiriwa na makundi yaliyojihami nchini Sudan Kusini
tangu mwanzo wa mwaka huu.
UNICEF
sasa ina hofu kuwa mzozo huo mpya huenda ukahatarisha maisha ya maelfu
ya watoo na kutaka shughuli hiyo ya kuwajiri watoto isitishwe mara moja.
Pia
inakadiriwa kuwa watoto 16,000 wameingizwa kwa makundi yaliyojihamia na
pia jeshini tangu mzozo nchini Sudan kusini uanze mwezi Disemba mwaka
2013.
Akiongea
baada ya kufanya ziara katika maeneo ya Bentiu na Juba nchini Sudan
Kusini, mkurugenzi mkuu wa UNICEF Justin Forsyth, alisema kuwa kuna hofu
kuwa huenda watoto zaidi wakaingizwa jeshini.BBC
0 comments:
Post a Comment