ikiwemo kujadili faida na changamoto za baadhi ya vifungu vya sheria hizo katika tasnia ya habari nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa MISA TAN,afisa Habari wa taasisi hiyo Jackline Jones ambaye pia ni mratibu wa mradi huo wa kuwajengea uwezo unaofadhiliwa na taasisi ya International Media Support(IMS) amesema lengo kuu la semina hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi hao ili kutambua maudhui ya sheria hizo.
“Tunachojaribu kupitia semina ni kuwaonesha na kuwasaidia Waandishi wapate Uelewa wa sheria ambazo zinasimamia tasnia yao.”Amebainisha Jackline
Afisa huyo amesema kupitia semina hiyo waandishi watakuwa na uwezo wa kushiriki mijadala mbalimbali ikiwemo ile ya mabadiliko ya baadhi yaa vifungu katika sheria hizo ambazo zinaonekana kuminya uhuru wa kujieleza.
Kwa upande wake mwezeshaji wa semina hiyo Jesse Mwandishi na Mhariri Mwandamizi Jesse Kwayu amebainisha kwamba yapo mambo mengi mazuri kwenye sheria za habari lakini mazuri hayo yanafunikwa na vifungu vichache vinavyominya uhuru wa habari na kujieleza.
Kwayu pia amewataka waandishi wa habari kuzisoma sheria hizo na kuzielewa ili wawe na uelewa juu ya vifungu mbalimbali katika sheria hizo.
"Sheria tulizonazo ukizisoma kwa wepesi utaziona ni nyepesi lakini ni sheria nzito sana,na Mwandishi ili akamilike lazima azifahamu sheria hizi"-amesema Kwayu
“Msione hili jambo ni la kwenu peke yenu,kama hivi MISA TAN walivyotushirikisha basi iwe fursa kwa taasisi nyingine za habari kuona umuhimu wa kushirikisha taasisi za kiraia ili kuunganisha nguvu na kuwa sauti ya pamoja.” Amebainisha Muhumpa.
0 comments:
Post a Comment