METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 6, 2021

MBEGU YA ALIZETI TANI 116 ZAWASILI TABORA

Mkuu wa  mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Burian akiwa anamkabidhi mfuko wa Mbegu za Alizeti kaimu mkurungezi wa manispaa ya Tabora Seif Salum kwenye kituo cha Reli Tabora.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Burian akiwa ameshikilia mfuko wa Mbegu ya Alizeti pembeni yake mkono wa kushoto aliyafaa suti ni Afisa Masoko wa Asa Emmanuel Luoga na katika ni katibu msaidizi huduma za Kilimo Raphael,Nyanda

Na Lucas Raphael,Tabora

Mkoa  wa  Tabora  umepokea shehena tani 116 za mbegu za alizeti  ikiwa  ni  mapokezi  ya  awali kati ya tani 240 ambazo  ni kwa ajili  ya  msimu  wa  Kilimo  wa mwaka 2021-2022

Alizeti hiyo ikiwa ni  utekelezaji wa Mpango wa Serikali wa kukabiliana na tatizo la upungufu wa mafuta  ya  kula nchini ambao umeelekezwa kutatuliwa kupitia kilimo cha alizeti.

Mkuu wa  mkoa wa Tabora Balozi Dr.Batilda Burian alisema kwamba kufika kwa shehena  hiyo ya Mbegu za alizeti kutoka Wakala wa mbegu  nchini ASA itawasaidia  wakulima  mkoani humo.

Mkuu huyo wa mkoa wa Tabora alipokea shehena hiyo jana  kwenye Kituo cha reli ya kati mkoani Tabora  kutoka kwa Wakala wa Mbegu nchini ASA .

Mkuu  wa  mkoa  wa  Tabora Balozi  Dr.Batilda Burian anakiri Shehena  hiyo ya Mbegu za alizeti itasaidia kwenye kilimo kufikia lengo la kukabiliana na tatizo la upungufu wa mafuta ya kula nchini

Hata hivyo aliwaagiza wakuu wa wilaya na Wakurugenzi kusimamia mbegu  hizo ili ziweze kuleta tija.

Awali afisa masoko wa wakala wa mbegu nchini kutoka mkoa wa shinyanga Emmanuel Luoga akizungumza kabla  ya kukabidhi shehena hiyo alisema kwamba mkulima akilima Mbegu hiyo  inauzao wa kumpatia magunia  kati ya gunia 7 hadi 11 zenye ujazo wa kilo 60 kwa ekari kulingana na huduma itakayotolewa wakati wa uzalishaji wake.

Aliendelea kusema kwamba wakulima walime mbegu hiyo kwa kufuata kanuni bora za kilimo na kuwahakikishia mavuno bora ambayo yataongeza upatikanaji wa mafuta mengi ya  alizeti nchi.

Alisema kwamba  wakala alipokea  mahitaji ya mbegu za alizeti (Standard seeds) kwa mkoa wa Tabora zaidi ya tani 208 Kwa kuanzia ASA wamekabidhi tani 116 kati ya mahitaji yaliyoombwa.

Katika msimu huu wa 2021/22, Wakala wa Mbegu za nchini ASA umepokea maelekezo ya Wizara juu ya maandalizi na usambazaji wa zaidi ya tani 2000 za mbegu ya alizeti inazotarajiwa kuwafikia wakulima katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwahi msimu wa Kilimo.

Serikali ilionesha Maeneo yakipaumbele   katika halmashauri za mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, Simiyu na Tabora.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com