METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 23, 2021

KIKAO CHA WATAALAMU CHAHITIMISHWA RASMI MJINI MOROGORO

Mratibu wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme wa Maji Julius Nyerere (JNHPP) kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Christopher Bitesigirwe akizungumza wakati wa kuhitimisha  kikao cha wataalamu, kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, na taasisi zilizopo chini ya Wizara hizo kimehitimishwa rasmi mjini Morogoro.

Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati(kushoto) Dkt. Richard Muyungi kutoka Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) wakiwa kikao cha wataalamu, kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, na taasisi zilizopo chini ya Wizara hizo kimehitimishwa rasmi mjini Morogoro.

Picha za Matukio mbalimbali wakati wa kuhitimisha rasmi kikao cha wataalamu, kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, na taasisi zilizopo chini ya Wizara hizo kimefungwa rasmi mjini Morogoro.

Hafsa Omar-Morogoro

Kikao cha wataalamu, kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, na taasisi zilizopo chini ya Wizara hizo kimehitimishwa rasmi mjini Morogoro.

Kikao hicho, cha kuandaa mkakati wa usimamizi wa rasilimali maji katika mabonde ya Rufiji na Pangani ili kuwezesha upatikanaji wa Nishati endelevu ya Umeme nchini, kilihitimishwa na Mratibu wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme wa Maji Julius Nyerere (JNHPP) kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Christopher Bitesigirwe.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhandisi Bitesigirwe aliwapongeza waatalamu hao kwa ushirikiano wao walionesha katika kipindi chote cha kufanya kazi hiyo.

Aidha, aliwataka kuendelea na ari hiyo ya ufanyaji kazi katika kipindi chote cha uaandaji na utekelezaji wa kazi hiyo mpaka pale itakapokamilika.

Pia, aliwasisitiza kutekeleza mambo yote ambayo kikao hicho kimeadhimia ili kuweza kufanikisha kazi hiyo ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa kiujumla.

Vilevile, aliwashukuru kwa kujitoa na kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanyika kwa mafanikio makubwa ambayo yatasaidia katika utekelezaji wake.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru sana, kwa michango na mawazo yenu, michango yenu hii ni muhimu sana hasa katika kuandaa huu mkakati wa usimamizi wa rasilimali maji katika mabonde ya Rufiji na Pangani,  michango hii itasaidia kuwezesha upatikanaji wa Nishati endelevu ya Umeme hapa nchini”alisema.

Kwa upande wake, Martha Ngalowera kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, alisema kuwa  mpango huo utakapo kamilika na kuanza utekelezaji wake utakuwa ni msaada mkubwa kwaajili ya kuzalisha umeme endelevu nchini.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com