Waziri wa TAMISEMI Innocent Banshungwa Akizungumza na wamachinga wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa soko la Mawamachinga Machinga Complec Dodoma hapo Jana.
Baadhi ya wanfanyabiashara na wananchi wakifuatilia hotuba ya viongozi waliotembelea mradi wa Ujenzi wa Soko la Machinga.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa akizungumza na viongozi na wamachinga Aliposhiriki kutembele mradi wa ujenzi wa Soko la Machinga Dodoma.
Mabango na Ramani za Mapendekezo ya namna Soko hilo litakavyokuwa wakati ujenzi utakapokamilika.
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa akiwa na Waziri wa Tamisemi wakizungumza jambo wakati walipoambana kutembelea mradi wa Ujenzi wa soko la wafanyabiashara wadogo ( machinga ) jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa ameielekeza Mikoa yote nchini kupitia Wakuu wa Mikoa kubuni maeneo ya machinga na kujenga miradi ya kuwapanga kulingana na mazingira ya Mkoa husika yatakayowaezesha wateja wao kuwafikia.
Waziri Bashungwa alieelekeza hayo jana Machi 09, 2022 wakati alipoambatana na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kutembelea mradi wa ujenzi wa Soko la Wafanyabiashara Wadogo (Machinga Complex) lililoko barabara ya Bahi Mkoani Dodoma na kuupongeza Mkoa huo kwa kutekeleza mradi rafiki wa mfano kwa wamachinga wa mkoa huo kupitia fedha za ndani.
Akifafanua Waziri Bashungwa alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshatoa bilioni 5 kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajiri ya kuboresha miundombinu na kuweka mazingira wezeshi ya Wafanyabiashara Wadogo (Machinga) nchini ambapo milioni 500 zimeletwa Dodoma Jiji.
Bashungwa aalieeleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI inaendelea kuwasiliana na wadau wa maendeleo na sasa ipo katika mazungumzo na Serikali ya India ili kuweza kupata fedha za kuongeza kwenye bilioni 5 zilizotolewa na Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwaajiri ya Wafanyabiashara wadogo.
Alieeleza kuwa tarehe 14 mwezi Machi 2022 amewaita Wakuu wa Mikoa wanaotoka kwenye majiji waambatane na Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Wakurugenzi ili kujadili na kupanga namna bora ya kujenga masoko ya wazi ya kisasa yatayoleta mageuzi makubwa kwa Wafanyabiashara Wadogo nchini.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema mradi huo utakapokamilika mwezi Mei, machinga wote walioko katika maeneo ya jiji la Dodoma watahamishiwa kwenye eneo hilo rasmi
0 comments:
Post a Comment