METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, December 29, 2021

DC MURO ' HII LAANA IMEENDA HADI KWENYE KUNDI MMEGAWANYIKA'







Na Hamis Hussein - Singida

Tofauti ya itikadi za vyama imetajwa kuwa ni sababu inayokabili kikundi cha maendeleo ikungi ambacho asili yake ni kundi sogozi ( whatsapp ambapo wajumbe wake wengi ni wazawa wa ikungi wakilenga kujadili maendeleo ya jamii zao kwa ujumla.

Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi katibu wa kundi la maendeleo ikungi Emanuel Mkonongo amesema kundi hilo limekuwa sehemu ya kuchangia harakati za amendeleo wilayani hapo ambapo kwa sasa limechangia fedha za ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari siuyu , kutengeneza madawati , kununua kalamu takribani 12000 kwa ajili ya wananfunzi wa wilaya hiyo. sanjari na hayo kundi hilo pia limekuwa sehemu ya faraja pale ambapo mwananchama anapopatwa na matatizo, mwenyekiti wa kundi hilo Simon mkongo ametaja baadhi ya changamoto kuwa ni umbali baina ya wanakikundi pamoja na itikadi za vyama jambo ambalo linakwamisha majadiliano ya maendeleo ya ikungi.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ikundi Jerry Muro Amesema tofauti ya itikadi baina ya wanakikundi imekuwa moja ya sababu inayopelekea kuwepo kwa mgawanyiko na kuongeza kuwa maendeleo ya ikungi hayataangalia kuwa wewe ni wa chama gani.
Mbunge wa jimbo la singida Mashariki Miraji Mtaturu akitoa salamu za wabunge amesema kundi hilo pamoja na mambo mengine limelenga kuongeza upatikanaji wa elimu na ujuzi kwa jamii ya ikungi ili kuwatengenezea fursa za kujikwamua kiuchumi na kusema kuwa kama kundi liatahakikisha linawasaidia vijana kupata elimu hasa ya ufundi stadi ili kujikwamua kimaisha.
kikao cha kundi la maendeleo ikungi kimefanyika mara ya tatu sasa hadi Kufikia jana desemba 28 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 kama kundi sogozi ( Whatsapp ) lilikotumika kama sehemu ya kubadilishana mawazo wakati wa vuguvugu la uchaguzi mkuu nchini Tanzania.

Tazama hapa jinsi DC wa ikungi Jerry Muro alivyowachana wanakikundi cha maendeleo , wenyewe wamekubali ni full vicheko aiseee!.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com