METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, October 8, 2021

ELIMU NA TANZANIA IJAYO

 Jesca Kishoa, Mbunge

Elimu ya msingi na sekondari sasa imetajwa kuwa elimu msingi. Serikali ilitekeleza azimio la kutoa elimu ya upili bila malipo. Hii ilifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache Africa ambazo 100% za gharama hubebwa na serikali. Kama ilivyo kwa Zimbabwe, Malawi, Lesotho na Kenya ambayo 2018 Bank ya Dunia iliitaja kama nchi kinara kati ya 43 kwa ubora wa elimu na bure. 2021 Shelisheli ni ya kwanza kwa elimu bora Africa, ya 28 duniani, watu wake wakiwa wameelimika kwa 95%.

Ripoti ya wizara ya fedha na mipango 2020 ilionesha kuwa idadi wa wanafunzi waliojiunga na elimu ya msingi iliongezekwa kwa *32%* , 2015 mpaka 2020, wakati sekondari ongezeko la wanafunzi ni *41%* , zaidi ya Tsh trillion *3.2* ziligharamia elimu.

Tanzania inatekeleza mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano 2021/25 ukilenga kujenga uwezo wa ushindani wa viwanda kwa maendeleo ya watu. Mpango huo utawezekana ikiwa tu tutatengeneza *RASILIMALI WATU* wenye *UJUZI* kwa kurekebisha mifumo yetu ya elimu, hii ni sababu iliyotajwa *Global Education System* kupelekea Tanzania kushika nafasi ya 16 kwa ubora wa elimu Afrika 2021. 

Ripoti ya jukwaa la kiuchumi duniani ( *World Economic Forum, 2017)* ilionesha kuwa *64%* ya watoto waliojiunga elimu ya msingi kwa mwaka huo, watafanya kazi ambazo kwa sasa hazipo duniani, hivyo elimu yetu ilenge kutoa ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira.

 *Mh. Rais Samia S. Hassan* akiwa Dar es Salaam (Tegeta) aliahidi kuwa makusanyo ya tozo ya mwezi septemba na oktoba yataelekezwa kwenye *UJENZI WA MADARASA*. Haya ni maendeleo makubwa sana ya KUJIVUNIA kama taifa.πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½.

Hata hivyo, pamoja na jitihada zinazofanywa, nchi imekuwa ikikumbwa na tatizo la kuzalisha wasimamizi zaidi kuliko watendaji. Hii inapelekea kuzorota kwa ujenzi wa uchumi wa nchi yetu kwakuwa nguvu kazi haikuandaliwa kwa uwiano sahihi, lakini pia hata hiyo nguvu kazi haikuivishwa ipasavyo kukabiliana na janga kubwa la umasikini.

Nchi zote tulizokuwa nazo sawa kimaendeleo mpaka miaka ya 1970 kama vile  Malaysia,  Singapore, Vietnam na Korea ya kusini, sasa zimetuacha; na  siri kubwa ya mafanikio yao ni uwekezaji kwenye kutengeneza rasilimali watu wenye weledi, ujuzi na maarifa ya  kubadilisha rasilimali vitu(maliasili) kuwa utajiri (wealth).  Kwa mfano, Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mpaka mwaka 1990, yaani miaka 30 iliyopita, nchi kama Vietnam ilikuwa na uchumi sawa na mataifa yetu ya Tanzania na Kenya. Mwaka 1990, uchumi wa Vietnam (Kwa maana ya Pato la Taifa) Ulikuwa Dola za Kimarekani  bilioni 8.4; Kenya Dola za Kimarekani bilioni 6.4 na Tanzania Dola za Kimarekani bilioni  4.5. Leo miaka 30 baadaye, uchumi wa Vietnam umefikia zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 270, Kenya Dola za Kimarekani bilioni 90 na Tanzania Dola za Kimarekani bilioni  64.  Kwa mara nyingine, siri kubwa ya Taifa hilo kuyaacha mataifa yetu kwa mbali ndani ya miaka 30 ni uwekezaji mkubwa kwenye kujenga nguvu kazi yenye maarifa na hivyo kuongeza uzalishaji viwandani na huduma

 *NINASHAURI* πŸ‘‡πŸ½;

 *1* . Rasilimali zaidi zielekezwe kwenye sekta ya elimu ili kuboresha miundombinu ya elimu.

 *2* . Wizara ya elimu iangalie upya mfumo wa elimu yetu( mtaala), ili elimu yetu iwe ya ujuzi zaidi (skills oriented).

 *3* . Rais ameonesha nia njema ya ujenzi wa madarasa, lakini ni muhimu pia kujenga na kuboresha MAABARA, mabweni na vifaa vya kujifunzia.

 *4* . Jamii ishirikishwe kwenye maboresho na maendeleo ya elimu. 

 *5* .    Serikali ibuni programu za kuongeza ufaulu kwa kuwaongezea wanafunzi muda wa kujisomea mpaka masaa ya jioni.  

#VisitTanzania2021
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com