Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wavuvi wa bwawa la mtera lililopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wavuvi 12 wamepoteza maisha na
wengine 15 kujeruhiwa katika kipindi cha mwezi wa pili 2020 hadi mwezi wa nane 2021
kufuatia matukio ya kuvamiwa na mnyama kiboko wakiwa ndani ya Bwawa hilo katika
shughuli zao za uvuvi.
Hayo yamezungumzwa katika Ziara
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ya kukagua Jitihada za Mamlaka ya Usimamizi
Wanyamapori Tanzania TAWA za kukabiliana na wanyama waharibifu na wakali
amewataka wavuvi kuzingatia njia sahihi za uvuvi salama ili kujilinda
Moyo alibainisha kuwa miongoni
mwa sababu za matukio hayo yalioondosha uhai ni pamoja na shughuli za Uvuvi
kufanyika kwenye mazizi ya viboko,tabia ya wavuvi kutumia zana dunu za
uvuvi,kupungua kwa samaki katika bwawa hilo na wavuvi kufanya shughuli ya uvuvi
nyakati za usiku ambapo viboko wanakuwa katika harakati za kutoka nje kutafuta chakula.
Moyo aliyetembelea Bwawa la
Mtera katika ziara ya kukagua jitihada za Ziara yake ya kukagua Jitihada za Mamlaka
ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania TAWA za kukabiliana na wanyama waharibifu na
wakali wakiwemo Viboko Na Tembo ameeleza kusikitishwa na matukio hayo huku
akitaja miongoni mwa sababu zinazochochea kuwapo kwa hatari dhidi ya wavuvi.
Aidha Moyo Amewaagiza maafisa
Uvuvi, viongozi wa Serikali kwa ngazi zote kusimamia na kuhamasisha
njia bora za uvuvi katika Bwawa la Mtera
ili kuepuka migongano ya Wanyama pori wakali na waharibifu akisisitiza kufuata
miongozo na kanuni za uvuvi
Lakini pia Moyo alisikitiswa na
vifo vya wafugaji watatu wanaoishi ndani ya hifadhi ya pori tengefu la Lunda
Mkwambi vilivyosababishwa na Tembo
wakati wakipita katika pori hilo la tukio hilo limekuwa kubwa kuwahi
kutokea katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa kuongezeka kwa
mtawanyiko wa tembo katika eneo la hifadhi ya Pori tengefu Lunda Mkwambi na
wafugaji kuishi porini humo na familia zao kunasababisha hatari ya maisha yao
kwa kuwa wanaishi mahali ambapo sio salama kwa maisha yao.
Wakitoa kero zao miongoni mwa
wavuvi wameeleza kuwa miongoni mwa sababu za kuendelea kuwapo kwa matukio ya
kuvamiwa na viboko ni ongezeko la wanayama hao katika bwawa hilo ambao wamekuwa
kero kwa wavuvi wa samaki katika bwawa la Mtera.
Walisema kuwa wanaiomba
serikali kuhakikisha wanawavuna viboko hao mara kwa mara ili kupunguza vifo na
majeruhi yanatokana na kuvamiwa na mnyama boko ambaye amekuwa tisho kwa maisha
ya wavuvi ambao wanafanya shughuli ya uvuvi katika bwawa hilo.
Waliomba serikali kuakikisha
wanaweka mbele maslai ya wananchi kwa kuwa ndio wanaojenga nchi kwa shughuli za
kiuchumi ambazo wamekuwa wakizifanya katika bwawa hilo la Mtera.
Akitolea ufafanuzi juu ya
malalamiko ya baadhi ya wavuvi Kamanda wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori
Tanzania TAWA Nyanda za juu kusini Joas Makwati alisema kuwa hawezi kuvuna
viboko wote bali kuna sheria na taratibu zinazowaongoza katika kuwavuna boko
hao.
Alisema kuwa hivyo wavuvi
wanatakiwa kutambua kuwa viboko wote wanaovunwa katika bwawa la Mtera huuzwa
kwenye mabucha mbalimbali kwa ajili ya kitoweo kwa wananchi kwa mjibu wa
taratibu na sheria za nchi zinavyotaka.
Makwati alisemuwa kuwa kwa mujibu wa Sensa iliyofanywa na Taasisi ya utafiti wa wanyama Pori Tanzania TAWIRI, Mwaka 2020 ilibaini kuwa bwawa hili linakadiriwa kuwa na voboko 261 sawa na asilimia 24 chini ya ustahimilivu wa Bwawa wa viboko 1070.
Aliongeza kwa kusema kuwa kwa
mujibu wa taratibu za TAWA za kudhibiti wanyama wakali na waharibifu unaendelea
kufanyika katika bwawa la mtera ambapo tangu mwezi wa pili 2020 hadi mwezi wa
nane 2021 jumla ya viboko 19 wamedhibitiwa kwa kuuwawa na kusaidia kupunguza
kadhia inayowapata wavuvi wanapofanya shughuli za uvuvi bwawani huo.
Makwati alisema kwa licha ya
changamoto hizo TAWA wamejipanga kuhakikisha wanaleta boti kwa ajili ya kuweka
kambi na kikosi cha kudumu Lunda mkwambi ili kuwa na muitikio wa haraka pindi
matukio hatarishi yanapojitokeza.
Alimalizia kwa kusema kuwa TAWA
inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi na njia za kuepukana na migongano kati ya
binadam na wanayamapori hao wakiwepo tembo na viboko.
Bwawa la Mtera lenye ukubwa wa kilometa za mraba 660 linapatikana ndani ya halmashauri za wilaya tatu, halmashauri ya wilaya Iringa, na upande wa MKOA WA Dodoma lipo katika halmashauri ya Mpwapwa na chamwino.
0 comments:
Post a Comment