Adeladius Makwega,WUSM-Dodoma
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imemkabidhi mkandarasa anayejenga jengo la wizara yao ambapo sasa vifaa vinatakiwa kuletwa katika eneo la ujenzi ambalo tayari limeshasafisha kwa kuanza kwa ujenzi huo.
Hayo yamebainika leo septemba 29, 2021 Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma ambapo zoezi la makabidhiano limefanyika mbele ya Wakala wa Majengo (TBA) na mkandarasi anayejenga jengo hilo Shirika la Nyumba La Taifa(NHC) jengo linalogharimu shilingi bilioni 22 na ushehe.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasimali Watu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Zahara Guga amesema kuwa makabidhiano yamefanyika kwa bashasha ya kila upande kuwa na shauku ya kuanza kwa kazi.
“Hatu zote za awali zilikuwa za kuhakikisha lengo la msingi ambalo ndilo ujenzi linafanyika, sasa ni wakati wa kutenda si wakati wa nadhari, sisi tunawakikishia kutoa ushirikiano wote kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi ulivyosainiwa.”
Manning Mwalwaka ambaye ni Meneja wa Huduma za Kihandisi wa NHC, ndiyo wanaojenga jengo hilo amesema kuwa ndani ya siku 14 vifaa vyote vya kisasa na mahitaji ya awali ya kuanzia ujenzi huo vitakuwa viko katika eneo la ujenzi na kazi itakuwa imeshaanza kwani sasa hakuna la kungoja.
“Katika zoezi hilo kuna changamoto ya mvua kubwa ambazo zinatarajiwa kunyesha wakati wa masika na maji yanaweza kutuama NHC tumejipanga kuleta vifaa vya kisasa ambavyo vitasaidia hata kuyaondoa maji yatakayotuama wakati wa kipindi cha mvua hizo.”
Mkadiliaji Majenzi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Peter Salyeem amesema TBA wanahitaji Wizara husika na NHC kufanya kazi kwa pamoja kwani hatarajii NHC ifanye kazi ya milioni 2, 3 au 10 iombe malipo angalau kazi yao ifanyike ya milioni 200 ukiomba milioni 190 hapo hakutakuwa na neno.
Katika makabidhiano hayo imebainika kuwa malipo ya awali yatakuwa ni asilimia 15 ya fedha ya ujenzi wa mradi wote na malipo mengine yanayofuata yatalingana na kazi itakavyofanyika.
Makabidhiano hayo yalishirikisha wakurugenzi kadhaa wa Wizara ya
Utamaduni Sanaa na Michezo, watendaji wa TBA na Watendaji kadhaa wa NHC.
Huku shabaha ya serikali katika ujenzi huo ni kukamilika ndani
ya miezi 24 baada ya kuanza kazi.
0 comments:
Post a Comment