Mashindano ya Mpira wa Miguu ya Angeline Jimbo Cup 2021 yanategemea kukutanisha timu za wanawake Kwa mara ya kwanza tangu Kuanzishwa kwake siku ya Jumapili ya Septemba 12, 2021.
Akizungumza wakati wa tukio la kukabidhi jezi kwa timu za wanawake zitakazoshiriki mashindano hayo Afisa Michezo wa Manispaa ya Ilemela Kizito Bahati Sosho amesema kuwa miaka yote tangu Kuanzishwa Kwa mashindano hayo yamekuwa yakizikutanisha timu za jinsia ya kiume tupu hivyo kutotoa fursa Kwa watoto wa kike wenye vipaji kuonyesha karama zao
'.. Tunamshukuru Mhe Mbunge Dkt Angeline Mabula ambae ndie muasisi wa mashindano haya Kwa kuona haja ya kuzikutanisha na Timu za wanawake katika mashindano haya, Wapo mabinti wengi wenye uwezo lakini walikuwa wakikosa fursa ya kuonyesha vipaji vyao ..' Alisema
Aidha Kizito amewataka watu wote wenye jinsia ya kike kuitumia vizuri fursa hiyo katika kushiriki na kuonyesha uwezo wao Kwa kuwa kitendo hicho kinaweza kutoa fursa ya kujikwamua kiuchumi Kwa kuajiriwa au kujiajiri kupitia sekta ya michezo tofauti na ilivyo Sasa ambapo mwamko umekuwa mkogo Kwa jinsia hiyo.
Kwa upande wake Bi Jamila kutoka kata ya Kirumba mbali na kushukuru Kwa hatua hiyo ya kutoa fursa ya ushiriki katika mashindano ya Angeline Jimbo Cup Kwa wanawake ameahidi kuahindi Kwa timu yake sanjari na kuwataka wadau na mashabiki kuwaunga mkono.
Wakati huo huo mchezo wa nusu fainali umeendelea siku ya Leo Kwa kuzikutanisha timu za kata ya Kirumba na Shibula ambapo Kirumba imeibuka kidedea Kwa kushinda magoli 3 Kwa sifuri na kufuzu kuingia hatua ya fainali.
0 comments:
Post a Comment