Chama cha Mapinduzi kimetoa rai kwa wakurugenzi wa halmashauri, miji, majiji na manispaa nchini kuhakikisha fedha za serikali zinazoletwa kwa lengo la kutekeleza miradi inayolenga kuimarisha huduma za wananchi na kusogeza huduma karibu zisiwe zinakaa muda mrefu kwenye akaunti, utekelezaji uwe wa haraka na ubora unaotakiwa ili wananchi waanze kunufaika kwa wakati.
Kimebainisha kuwa baadhi ya Halmashauri za miji, majiji na manispaa hapa nchini zinazo fursa na vyanzo vizuri vya kukusanya mapato lakini kukosekana kwa ubunifu, uadilifu na ushirikiano baina ya mkurugenzi, wataalam, madiwani na kamati za ulinzi na usalama wameishia kukusanya chini ya kiwango na kutaka kutegemea serikali kuu kwa kila kitu
Katibu wa Halamshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ametasema hayo mara baada kukagua ujenzi wa jengo la utawala halmashauri ya mji wa Tunduma na ujenzi wa kituo cha chipaka ikiwa ni ukaguzi wa miradi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
"Hata wale ambao wanakusanya vizuri baadhi ya maeneo wameshindwa kusimamia matumizi yake kuhakikisha yanakwenda kwenye vipaumbele vinavyolenga kuwaondolea kero wananchi kama chama kilivyoelekeza kupitia ilani yake ya uchaguzi 2020-2025 alisema Shaka.
Shaka amesifu juhudi zinazochukuliwa na halmshauri hiyo katika kusimamia matumizi ya fedha katika kutatua kero za wananchi na kuimarisha huduma za kijamii, kadhali wakijitahidi kutekeleza miradi ya maendeleo kwa uweledi, uaminifu na ungalifu mkubwa hasa fedha za serikali kuu.
"Halmashauri ya mji wa Tunduma ni mfano mzuri wa kuigwa mhe Rais Samia mnatendea haki katika eneo hili nimpongeze mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji Bi. Regina Bieda wataalam wake, madiwani na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Momba kwa namna wanavyosimania ukusanyaji mzuri wa mapato ya Serikali pamoja na matumizi" Alifahamisha Shaka
0 comments:
Post a Comment