Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akisiliza maelekezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Iramba, Mkoani Singida wakati alipotembelea chumba cha
upasuaji Hospitali hapo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa vya Maabara
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Wilaya ya Iramba namna wanavyokusanya mapato.
Jengo la Utawala la Hospitali ya wilaya ya Iramba na juu ni baadhi ya majengo ya Hospitali hiyo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni kwenye Zahanati hiyo
Kisimba
Jengo la Zahanati ya Kisimba
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akisalimia wenyeji (Hawapo pichani) wakati
alipotembelea Zahanati hiyo ya Kisimba
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akisalimiana na watumishi wa Zahanati hiyo ya
Kisimba.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha dawa kwenye Zahanati hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika
Wilaya Iramba Mkoani Singida na kukagua huduma za Afya katika Hospitali ya
Wilaya pamoja na Zahanati ya Kisimba ndani ya Wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameweza kubaini
mapungufu mbalimbali ambayo ameagiza yapatiwe ufumbuzi ndani ya miezi mitatu.
Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ameweza
kujionea huduma mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo hata hivyo ameagiza
uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanafunga mfumo wa ukusanyaji mapato wa
malipo wa kisasa kwa njia ya kielektroniki.
“Mfumo wa malipo ya kielektroniki umeleta ukombozi
mkubwa sana kwenye mahospitali nchini. Mapato yameongezeka. Udhibiti wa mapato
umekuwa rahisi. Nawaagiza nanyi Hospitali ya Iramba kuhakikisha munafunga mfumo
huu wa malipo wa kisasa hususani kwenye: Maabara,Chumba cha upasuaji (Theatre),
Dirisha la dawa, na sehemu zote zenye kuingiza mapato”. Ameeleza Dk.Kigwangalla
wakati wa kutoa maagizo hayo.
0 comments:
Post a Comment