Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
ameupongeza Umoja wa waendesha bodaboda Jijini hapa kwa kuchangia mifuko
75 ya sementi kwa ajili ya ujenzi wa wodi za watoto katika hospitali
ya kanda ya Rufaa ya Mbeya.
Waziri
Ummy ametoa pongezi hizo wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi la
ujenzi wa wodi tatu ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
mrundikano wa watoto katika hospitali hiyo
“Kwa
niaba ya Serikali nawashukuru wadau wote waliochangia ujenzi huu ila
niseme nimevutiwa sana na mchango wa Umoja wa waendesha Bodaboda kwa
kushiriki ujenzi huu, mmefanya jambo jema na la Kizalendo katika
kutatua changamoto za utoaji huduma za afya kwa watoto katika hospitali
hii ambayo inahudumia mikoa saba” alisema.
Aidha,Waziri
Ummy ametoa rai kwa makundi mengine ya kijamii hususan wa kanda ya juu
kusini kuiga mfano huo mwema wa bodaboda katika kuchangia kukamilisha
ujenzi huo ili ifikapo Januari,2017 jengo hilo lianze kutumika .
Wakati
huohuo Waziri huyo amewaagiza Waganga wakuu wote wa Mkoa na Wilaya wa
hospitali za Umma nchini kuhakikisha wanatumia vizuri rasilimali
zilizopo katika maeneo yao ili kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili katika utoaji huduma za afya kwa wananchi badala ya
kusubiri fedha kutoka Serikali Kuu.
“Serikali
imedhamiria kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa kwa wananchi wa
kanda za juu kusini tumejipanga kuhakikisha kuwa ujenzi wa jengo la
uchunguzi (Diognistic Centre) lililokwama kwa takribani miaka saba
unakamilika ndani ya mwaka mmoja”,hii itawaondolea kero wananchi wa
nyanda hii kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya huduma za vipimo vya
kiuchunguzi wa magonjwa kama TC Scan
Kuhusu
matibabu ya saratani kwa njia ya dawa (Chemotherapy Waziri Ummy alisema
matibabu hayo yataanza kutolewa mapema mwakani na hivyo itapunguza kero
kwa wananchi wa kanda ya Mbeya kwenda katika hospitali ya saratani ya
Ocean Road.
Awali,
akitoa taarifa ya ujenzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Kanda
ya Rufaa Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji alisema ujenzi wa wodi hizo ambao
utagharimu shilingi milioni 300 ambazo zinatokana na fedha za ndani za
hospitali hiyo pamoja na michango ya wadau wa maendeleo wa Mkoa wa
Mbeya.
0 comments:
Post a Comment