Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, Tarehe Juni 23 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe kutoka Brazil Paulo Pan (International Promotion Through Sports) na Flavio Pazeto (Ubalozi wa Brazil) juu ya maendeleo ya michezo nchini Jijini Dodoma wakiwa katika ziara ya kwenda kutembelea kituo ya Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza.
Katika
mazungumzo hayo Mhe. Bashungwa ameshukuru Ubalozi wa Brazil nchini Mhe. Antonio
Augusto Cesar na Serikali yao kiujumla kwa kuitikia wito wa kikao kilichokaliwa
Mei 21 2021 Jijini Dar es Salaam kati yake na Balozi wa Brazili Nchini
kilichokuwa kimelenga hasa Maendeleo ya Michezo nchini hasa katika upande wa
soka na Mchezo wa Masubwi kwa kufanya Programu ya kubadilishana wakufunzi.
Mhe. Waziri amekubaliana na ujumbe huo kuanzisha Memorandum kati ya Wizara na Paulo Pan kutoka International Promotion through Sports kwenye kuendeleza sekta ya michezo Nchini.
Makubaliano hayo ambayo watakaa kati ya International promotion Through Sports na Wizara yatatoa fursa ya kukutana na Kamati ya Olipic ya Dunia na Shirika la UNESCO ili kuangalia namna ya kutunisha mfuko wa maendeleo wa michezo Nchini.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment