UMOJA wa vijana wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa Vijijini (UVCCM) wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia suluhu Hassan kwa kuongeza fursa za kiuchumi kwa vijana wa kitanzania na kuijenga Tanzania mpya ya Vijana
akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa umoja wa vijana wilaya ya Iringa Vijijini,Makala mapesah alisema kuwa Rais wa awamu ya sita anakwenda kuijenga Tanzania ya vijana itakayodumu kwa miaka zaidi ya hamsini kwa kuwa na vijana ambao watakuwa na uwezo wa kuishauri serikali,kuwa vijana hodari wa kuhoji,kukosoa na kujenga nchi.
Alisema kuwa vijana wengi sasa watazijua fursa nyingi zilizopo katika uongozi serikali ya awamu ya sita ambazo zitasaidia vijana wengi kujikomboa kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi kwa wazazi au kuomba omba bila ya sababu yoyote ile.
Mapessah alisema kuwa seikali ya awamu ya sita imetengeneza fursa mbalimbali kwenye kila sekta kwa ajili ya kuwakomboa vijana kiuchumi na kuacha kutegemea kuajiliwa badala yake waweze kujiajili wenyewe.
alisema kuwa Rais wa awamu ya sita ameamua kuhakikisha anaondoa chuki zilizokuwepo kwa vijana ambao wanaitikadi tofauti ya vyama na kuwajengea kuwa wamoja jambo ambalo litasaidia kuwa na viongozi vijana wazuri watakao dumu kwa zaidi ya miaka ishirini hadi hamsini hapo baadae.
Mapessah alisema kuwa kitendo cha Rais kukutana na kuongea na vijana kumetoa fursa kuwa kwa vijana kuona kuwa nao sasa wameanza kuthaminiwa na serikali ya awamu sita ambapo hutuba yake imejaa matumaini kwa vijana kwa kuijenga Tanzania mpya.
Alimalizia kwa kuwaomba vijana wote nchini kumuunga mkono Rais wa awamu ya Sita kwa kuwa ameonyesha maono ya kujijenga Tanzania mpya ambayo kila mtanzania anatarajia kuiona na kuwa na matumaini nayo ya kimaendeleo.
0 comments:
Post a Comment