JIJI la Dar es Salaam ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi barani
Afrika na ukuaji wake kuathiri sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi
hasa usafiri na usafirishaji.
Tangu miaka ya 1990 kumekuwa na mipango mbalimbali ya kuboresha usafiri
Dar es Salaam ikiwamo kuanzisha barabara za aina mbalimbali, kama za
mabasi yaendayo kasi, maegesho ya magari ya kulipia na kuhamasisha
kujengwa kwa majengo yenye maegesho ya magari.
Pamoja na jitihada za serikali ya jiji na serikali kuu kuboresha usafiri
bado kuna kero kubwa ya usafiri wa abiria, hasa wakati asubuhi na jioni
hali inayowalazimu wananchi kuchukua takribani saa tatu barabarani
badala ya dakika 15 hadi 30 , kwa mfano, kutoka Mbezi ya Barabara
Morogoro hadi katikati ya jiji na Kariakoo.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo, tangu mwaka 2008 Wakala wa Barabara
Nchini (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam imetekeleza miradi maalum ya
ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano katika barabara kuu za jiji.
Mhindisi Miradi wa Ofisi ya Tanroads Mkoa wa Dar Es Salaam, Julius
Ngusa, anasema mradi wa ujenzi wa barabara za pembezoni wa awamu ya tatu
ni moja ya mikakati ya serikali ya kushughulikia tatizo sugu la
msongamano wa magari ambapo utekelezaji wake ulianza tangu 2008/2009.
Anasema kupitia mradi huo, serikali ilichagua barabara tisa kwa ajili ya
kujengwa katika viwango vya lami nazo ni barabara ya Ubungo (bus
terminal)-Kigogo-Kawawa yenye kilometa 6.4, barabara ya Jet
Corner-Vituka-Davis Corner urefu wa kilometa 12, nyingine ni
Kinyerezi-Kifuru-Msigani-Mbezi Mwisho yenye kilometa 10.
Barabara ya Mbezi- Goba- Tangibovu yenye kilometa tisa, kadhalika ya
Kimara Baruti-Msewe-Changanyikeni yenye urefu wa kilometa 2.6.
Ngusa, anazitaja barabara nyingine kuwa ni pamoja na Tegeta Kibaoni-Wazo
Hill-Goba-Mbezi ndani ya Morogoro yenye kilometa 20, Kigogo
Roundabout-Jangwani-Twiga katika bonde la Msimbazi ikiwa na kilometa
2.72.
Anazungumzia pia Tabata Dampo-Kigogo na Ubungo Maziwa- Mabibo External inayoingia Mandela inayojengwa kilometa 2.25 za lami.
“Miradi hiyo inajengwa katika awamu tatu za utekelezaji, ambapo hadi
sasa awamu ya kwanza ya miradi hiyo iliyohusisha ujenzi wa barabara
zenye jumla ya kilometa 19.42 tayari imekwishatekelezwa na kukamilika
tangu 2008.”
Anaitaja miradi iliyokamilika kuwa ni pamoja na barabara ya
Ubungo-Kigogo-Kawawa iliyokamilika mwaka 2010 kwa gharama ya Sh bilioni
11.44, Kigogo-Msimbazi-Jangwani iligharimu bilioni 7.64 ambayo
ilikamilika mwaka 2017 pamoja na barabara ya Jet Corner-Vituka-Devis
Corner iliyomalizika mwaka 2011.
“Kuhusu awamu ya pili yenye urefu wa kilometa 27.5 na ujenzi wa daraja
la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40, kazi ilianza mwaka 2014 ambako hadi
sasa zilizojengwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara ya Tangi
Bovu (Samaki)-Goba iliyomalizika mwaka jana na kugharimu bilioni 8.6 ”
anasema Ngusa.
Katika awamu hiyo mwaka 2016 serikali pia ilikamilisha ujenzi wa
Barabara ya Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba-Mbezi Mwisho yenye kilometa
20, kwa gharama ya Sh bilioni 6.7.
Akifafanua zaidi Ngusa anasema miradi mingine iliyokamilika ni pamoja na
Barabara ya Kilungule (Maji Chumvi)- External/Mandela yenye kilometa
3.3, ambapo mradi huo ulikamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Sh. bilioni
4.4.
Aidha mradi wa barabara ya Kimara Baruti-Msewe wenye kilometa 2.6
uliopaswa kukamilika mwaka jana umeshindishwa kuisha kwa wakati kutokana
na kutokuwepo kwa nafasi ya kujenga barabara, ambapo hata hivyo hadi
kufikia 30 Septemba, 2017 mradi huo ulijengwa kwa asilimia 80.
Mhandisi Ngusa anasema awamu ya tatu ya utekelezaji wa miradi hiyo
ulioanza mwaka 2016 na 2017 unahusika ujenzi wa barabara za
Kifuru-Msigani, Goba-Makongo na Goba-Madale zenye urefu wa kilometa 14.1
na unatarajia kukamilika mwanzoni na nyingine mwishoni mwa mwaka 2018.
“Miradi ya barabara ya Goba-Madale na Goba-Makongo hadi kufikia Septemba
30, mwaka huu imekamilika kwa asilimia 52 wakati ule wa Kifuru-Msigani
umefikia asilimia 87, malengo ni kuhakikisha kuwa miradi hii inamalizika
kwa wakati kwa kuzingatia ubora na viwango tulivyojiwekea” anasema
Ngusa.
Baadhi ya changamoto inayokabili miradi hiyo ni pamoja na wamiliki wa
nyumba nyingi kuhitaji fidia, ambapo Tanroads kwa kushikiana na Wakala
wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) zimeanza uthamini na malipo
yatalipwa na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi).
Anasema serikali pia inaendelea na ujenzi wa barabara za Msongola-Mbande
zenye kilometa moja nyingine ni Ununio-Mbweni urefu wa kilometa moja
pia , Kitunde-Kivule yenye urefu wa kilometa 3.2, pia kilometa nyingine
moja zinajengwa za barabara ya Dege-Gomvu.
Kukamilika kwa miradi hii kutaongeza tija na ufanisi katika kuchochea kasi ya maendeleo ya Dar es Salaam na taifa .
Saturday, October 7, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
HOTUBA YA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA JIMBO LA ISIMANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI MWAKA 2015 UTANGULIZI UTA...
-
Na Debora Charles (Mtakwimu) Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusamba...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment