METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, June 2, 2021

MBUNGE WA ROMBO NA WAZIRI WA KILIMO PROF MKENDA AGAWA BAISKELI ZA WALEMAVU KWA AWAMU YA PILI JIMBONI KWAKE ROMBO



Na Mwandishi Wetu, Rombo


Mbunge wa jimbo la Rombo ambaye ni Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda ametoa baiskeli 10 za walemavu katika jimbo lake la Rombo kama sehemu ya ahadi zake za kusaidia makundi maalumu katika jamii.


Katika awamu ya kwanza, Prof. Mkenda alitoa baiskeli 5 na awamu hii pia ametoa baiskeli 5 baada ya kuona kuwa bado kuna uhitaji wa baiskeli hizo.


Baiskeli hizo zimekabidhiwa kwa wahitaji kupitia kwa madiwani wa kata wanazotoka ili ziweze kuwafikia kwa urahisi.


Wakizungumza baada ya kupokea baiskeli hizo, madiwani wa kata zilizopekea baiskeli hizo wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuendelea kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalumu kwani wamekuwa katika kundi lenye changamoto nyingi na hivyo kuhitaji msaada kutoka kwenye jamii ili kukabiliana na changamoto hizo.


Mwananchi mmoja mwenye ulemavu wa viungo ndugu Karoli Lyakurwa aliyefika na diwani wake kupokea baiskeli yake kutoka kwa Mbunge amesema kuwa "Ninamshukuru sana Mbunge kwa kutukumbuka sisi walemavu kwani tumekuwa tukisahaulika sana"


MWISHO



Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com