Mshauri mwandamizi kutoka Shirika la UN Women, Bi. Usu Mallya (kulia) akiwasilisha mada kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.
Mwanaharakati mkongwe Gema Akilimali (kushoto) akiwasilisha mada
kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania 2017. Wengine ni maofisa maendeleo ya
jamii wakifuatilia.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017.
Mwanaharakati na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT),
Mary Rusimbi akizungumza kwenye moja ya warsha katika Tamasha la Jinsia
Tanzania 2017.
KUANZIA Septemba 5 hadi 8, 2017 Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa
masuala ya jinsia iliadhimisha siku nne za Tamasha la 14 la Jinsia
Tanzania. Siku hizo nne ziliambatana na shughuli za sherehe, tafakuri,
mijadala na pongezi. Baada ya kumalizika kwa shughuli zote hizo TGNP
Mtandao na wadau washiriki katika tamasha walitoka na mikakati kadhaa
kukabiliana na changamoto zilizoibuliwa.
Bi. Vicensia Shule ni Mwenyekiti wa Bodi
ya TGNP Mtandao, anasema baada ya tamasha hilo mikakati waliojiwekea
kukabiliana na changamoto zilizoibuliwa ni pamoja na kushirikisha wadau
mbalimbali zikiwemo AZAKI, wadau wa maendeleo, asasi za elimu ya juu na
taasisi za Serikali katika kutafuta na kufanya uchambuzi ili ili kupata
taarifa na takwimu sahihi juu ya mimba na ndoa za utotoni, ukatili wa
kijinsia na umiliki wa ardhi kwa wanawake na watu wenye ulemavu.
Anasema pia wataendelea kuimarisha
mikakati ya kuweka kumbukumbu za wanawake waliotoa michango katika
maendeleo kwenye nyanja mbalimbali na kusambaza taarifa za kumbukumbu
hizo kwa ajili ya watu kujifunza na kuwaenzi wanawake hao. Pia kupanua
wigo wa kutoa mafunzo ya kimwongozo katika kuchukua na kuhifadhi
kumbukumbu za wanawake kwa AZAKI, vijana na wadau wengine.
Aidha Bi. Vicensia Shule anaeleza kuwa
mikakati mingine ni kuweka mipango endelevu wa kurithisha ujuzi na
maarifa kutoka kizazi/rika moja kwenda nyingine, hasa kutoka kwa
wanawake waliobobea kwenye tasnia mbalimbali.
Pamoja na hayo anasema mkakati mwingine
ni kushinikiza sera na mipango ya Serikali iingize masuala ya vijana ili
waweze kushiriki kikamilifu katika maendeleo nyanja zote, hii ni kwa
kuwa zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania ni vijana. Watashawishi pia
rasilimali za kutosha zitengwe ili kuwezesha utekelezwaji wa mipango na
mikakati ya vijana bila kujali itikadi, jinsi, dini, jiografia na hali
ya kipato.
Baadhi ya washiriki kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017.
Baadhi ya washiriki kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017.
Baadhi ya washiriki kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Mbeya, Zena Kapama
akizungumza katika moja ya warsha kwenye Tamasha la 14 la Jinsia
Tanzania.
Mratibu wa MVIWATA Kyela, Bi. Theodora Pius akichangia hoja katika Tamasha la 14 la Jinsia Tanzania.
Mjumbe Kamati ya Ushauri katika Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Dk.
Dinah Mmbega akichangia hoja kwenye moja ya warsha katika Tamasha la
Jinsia Tanzania 2017.
0 comments:
Post a Comment