METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, April 17, 2021

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI NDG GERSON MSIGWA AKEMEA MANYANYASO KWA WAANDISHI WA HABARI NCHINI

Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg Gerson Msigwa akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Mtangulizi wake Dkt Hassan Abass, Tarehe 17 Aprili 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg Gerson Msigwa akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Mtangulizi wake Dkt Hassan Abass, Tarehe 17 Aprili 2021.

Na Mathias Canal, Dodoma

Serikali imesema haitokubali waandishi wa habari nchini kunyanyawaswa kwa namna yoyote ile.

Kauli hiyo imetolewa tarehe 16 Machi 2021 na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg GERSON MSIGWA mbele ya waandishi wa habari Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Mtangulizi wake Dkt Hassan Abass ikiwa ni mwanzo rasmi wa majukumu yake mapya.

Pia, Msigwa ametoa angalizo kwa waandishi wa habari kuzingatia  sheria, kanuni na miongozo inayoongoza tasnia ili kuepuka sintofahamu inayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Pamoja na kuwataka waandishi wa habari nchini kutotumika kuibomoa nchi yao pia ametoa mwito kuhakikisha wanakuwa vinara wa kuijenga Tanzania.

Kwa upande wake aliyekuwa msemaji mkuu wa Serikali Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Hassan Abass amewashukuru waandishi wa habari, Wadau na Watanzania wote kwa ujumla kuunga mkono juhudi za serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com