METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 3, 2021

RC HOMERA AANIKA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOANI KATAVI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera akielezea fursa za Uwekezaji zilizopo katika Mkoa huo wakati wa Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Katavi, Hafla inayofanyika katika Ukumbi wa Mpanda, Leo tarehe 3 Machi 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Katavi, Hafla inayofanyika katika Ukumbi wa Mpanda, Leo tarehe 3 Machi 2021.

Wawekezaji  waliohudhuria uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji mkoani katavi wametakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji katika mkoa huo wenye zaidi ya hekta 45,000.

Akizungumza katika mkutano huo uliowakutanisha wadau wa uwekeaji kutoka maeneo mbalimbali, Mkuu wa mkoa huo Mhe Juma Homera amesema katika ujenzi wa viwanda mkoa umetenga hekari 245 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda mbalimbali.

“Kutokana na wingi wa samaki wanaovuliwa kutoka ziwa Tanganyika wakiwemo, migebuka, kuhe, sangara pamoja na kamongo, mkoa umetenga hekari 245 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kusindika na kuchakata  samaki” Amekakaririwa Homera

Homera ameongeza kuwa wawekezaji wanayo fursa ya ujenzi wa viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya usindikaji nafaka, ujenzi wa viwanda vya asali, uchakataji wa nyama na maziwa, pamoja na viwanda vya mbao.

Katika sekta ya utalii Homera amesema wawekezaji wanayofursa ya kuwekeza katika upande wa makampuni ya utalii yatakayosaidia ongezeko la utalii katika mkoa huo, wenye vivutio vingi va utalii ikiwemo mto mapacha ,mto maji moto pamoja na hifadhi ya taifa katavi yenye ukubwa wa hekari 4471.

“Tuna zaidi ya sokwe 2500, tuna tweiga mweupe ambae huwezi kumpata kokote Tanzania isipokuwa mkoani katavi, lakini pia tunao viboko  na tembo wakubwa sana kama nyumba” Amesema

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com