METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 3, 2021

KAMA KUNA AKILI YA UWEKEZAJI BASI IKO KATAVI- PROF MKUMBO

 

Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera wakionyesha vitabu vya Uwekezaji mara baada ya kuzindua Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Katavi, Leo tarehe 3 Machi 2021.

Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Katavi, Leo tarehe 3 Machi 2021.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Katavi, Leo tarehe 3 Machi 2021.

Watumishi wa umma popote walipo nchini wametakiwa  moja ya kazi zao za msingi  iwe ni kuwawezesha na kuwasaidia watu na makampuni yanayotaka kuwekeza kufanya shuhuli zao bila bugudha yoyote.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo Mkoani Katavi  katika mkutano wa  uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji mkoani humo uliowakutanisha wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali.

“Kila siku tunasisitiza, mtumishi wa Umma ukitaka serikali ikuhudumie vizurilazima uwaheshimu na kuwathamini wawekezaji na yeyote anaye wanyanyasa na kuwadharau wawekezaji basi hajitambui” Amekaririwa Prof Mkumbo

Aidha, Prof Mkumbo amewataka wananchi kuondoa dhana ya kuwa uwekezaji ni suala linalofanywa na wageni tu, badala yake amewataka watu binafsi  na makampuni binafsi na hata wanafunzi wa vyuo vikuu  kujitokeza  kwa kuwa na mtaji, kufanyabiashara na kupata faida.

Muwekezaji sio lazima awe ni mtu tajiri sana au kutoka nje ya nchi, La hasha, hata wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali wana uwezo wa kuwa wawekezaji kwa kuweka akiba kutoka kwenye fedha zao za kujikimu na mwisho wa masomo anaweza akawa muwekezaji mkubwa” Amesisitiza

Hata hivyo Prof. Mkumbo pia amewataka wawekezaji kutimiza majukumu yao ya msingi ikiwa ni pamoja na kuwapa stahiki zao ikiwemo mikataba kwa wafanyakazi wao pamoja na  kushiriki kujitoa katika huduma za kijamii.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com