Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akituma salaam kwa wana Dar es Salaam, Tanzania na Afrika kwa ujumla kuwa Tamasha la Serengeti Music Festival kuwa limewadia na litafanyika tarehe 26,Desemba 2020 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya tamasha hilo.
Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva Khalid Mohamed
maarufu kama TID akiwahakikishia mashabiki zake kuwa amejipanga kutoa burudani
ya viwango vya hali ya juu hivyo wasanii wengine nao wajipange kwani hili ni
tamasha kubwa sana na watanzania wanatarajia show nzuri, leo Desemba 24, 2020
Jijini Dar es Salaam, katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia
maandalizi ya tamasha la Serengeti Music Festival.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi ametuma salamu kwa Wana Dar es Salaam, Watanzania wote na Afrika kuwa Tamasha la Serengeti Music Festival limewadia na litafanyika Desemba 26, 2020 Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Desemba 24, 2020 alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Serikali kwa lengo la kuanzisha uhusiano wa karibu kwa sekta ya Sanaa na Utalii.
Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Dkt. Abbasi alisema tamasha hilo litakua ni shukran ya mchango wa wasanii wazamani ambao wamesaidia ukuaji wa tasnia ya Muziki nchini kutoka kuonekana kama jambo la kihuni mpaka kuonekana kuwa chanzo cha kuchangia pato la mmoja mmoja na taifa.
"Serikali imesikia kilio cha Wasanii wengi kuhusu Taifa kutokuwepo kwa tuzo zinazoandaliwa hapa nchini hivyo basi mwezi Machi, 2021 tutakuwa na Tuzo. Tutaanda tuzo hizo na Wasanii tunaomba kwa atakayeshindwa basi akubali na asiende kulalamika popote" alisema Dkt. Abbasi.
Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali alisema baada ya Tamasha hilo, tarehe 27, Desemba 2020 kutakuwa na mwendelezo wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni litakalofanyika Bagamoyo katika chuo cha TaSuBa, na huko kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo ngoma za asili.
Naye Msanii wa Hip Pop Kala Jeremiah ameishukuru Serikali kwa kuandaa tamasha hilo, huku akisema anaamini kuwa tamasha hilo limeanzishwa katika kipindi cha sherehe za Krismas litaendelea kuwa tamasha kubwa hapa nchini na Afrika.
Halikadhalika kwa upande wa Msanii Khalid Mohamed maarufu kama TID alitoa shukran kwa Serikali nakuwahakikishia watanzania kuwa amejipanga kutoa burudani ya uhakika hivyo mashabiki zake wasikose kufika uwanjani siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment