METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 24, 2020

AGIZO LA RC KUNENGE KWA MACHINJIO YA VINGUNGUTI LATEKELEZWA, JARIBIO JINGINE LA UCHINJAJI LAONYESHA UFANISI


Kufuatia maagizo aliyotoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge kwa machinjio ya kisasa Vingunguti kuhakikisha wanarekebisha kasoro zilizoonekana kwenye jaribio la kwanza la uchinjaji ikiwemo kasi ndogo ya uchinjaji, kukosekana kwa elimu ya matumizi ya mitambo, hatimae leo jaribio jinginge la uchinjaji limeonyesha ufanisi.

RC Kunenge akiongozana na Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo wamefika na kujionea vijana wa kitanzania wakifanya zoezi la kuendesha mitambo hiyo baada ya kupatiwa elimu ya matumizi ya mitambo hiyo Jambo lililosaidia kuongezeka kwa kasi ya uchinjaji.

Akizungumza baada ya kujionea zoezi hilo RC Kunenge amesema kasi ya uchinjaji kwa siku ya Leo imeonyesha matokeo mazuri lakini bado yapo mapungufu madogomadogo yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho.

Aidha RC Kunenge amewaelekeza wahusika wa Mradi huo kuhakikisha elimu inaendelea kutolewa kwa vijana hao ili waendelee kupata uzoefu wa kutosha.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amesema machinjio hiyo itatoa ajira kwa vijana zaidi ya 300 na itakuwa na uwezo wa kuchinja Ng'ombe 1,000 kwa siku, Mbuzi 1,000 na Kondoo 1,000 ambapo zoezi la uchinjaji wa Ng'ombe mmoja linachukuwa takribani Dakika 15.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com