Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally, Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wakati alipotembelea Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam ambao umekamilika kujengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco wakati akielekea Mburahati kwa ajili ya Mikutano ya Kampeni za Urais kwa upande wa Chama cha Mapinduzi CCM leo tarehe 13 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati alipotembelea Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam ambao umekamilika kujengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco baada ya Mhe. Rais Magufuli kumuomba Mfalme wa Morocco kuwajengea Waislamu Msikiti alipofanya ziara hapa nchini tarehe 24 Oktoba, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wakati alipokuwa akielezea ujenzi huo wa Msikiti mpya uliokamilika kujengwa katika Makao makuu ya Bakwata Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally wakati alipotembelea Msikiti huo Mkuu wa Bakwata Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua iliyokuwa ikiongozwa Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally mara baada ya kutembelea Msikiti Mkuu wa Bakwata uliokamilika kujengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally, Balozi wa Morocco hapa
nchini Abdelilah Benryane wakwanza kushoto, pamoja na viongozi mbalimbali wa
Bakwata mara baada ya kutembelea Msikiti Mkuu wa Bakwata uliokamilika kujengwa
kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco. PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment