Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA Imani Nkuwi alipowasili Mkoani Tabora.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA Imani Nkuwi akisalimiana na wafanyakazi wa TAWA Tabora
Askari wa TAWA wakisimsikiliza Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA Imani Nkuwi.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA Imani Nkuwi amewataka wafanyakazi wa Mamlaka kufanya kazi kwa uzalendo, ueledi na kudumisha upendo miongoni mwao ili kuiwezesha TAWA kufikia malengo yake waliyokusudiwa
Nkuwi ametoa wito huo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Tabora na kufanya mazungumzo na watumishi wa vituo vilivyochini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) vilivyopo Mkoani humio.
Vituo hivyo ni pamoja na Kanda Dhidi ya Ujangili ya Magharibi (KDU),Pori la Akiba la Ugalla,Pori la Akiba Luganzo Tongwe na Pori la Akiba Wembere
katika Ziara hiyo pamoja mambo mengine Naibu Kamishna Nkuwi alitoa ufafanuzi kwa watumishi hao kuhusu mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali katika Shirika pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakibili watumishi kwenye vituo vyao.
Naibu Kamishna Nkuwi alitumia fursa kuwaasa watumishi kuzingatia tunu za TAWA zilizoanishwa katika Mpango Mkakati wa TAWA katika kutekeleza majukumu yao.
Aidha aliwaasa watumishi kujiepusha na kushawishika kupokea rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha haki na sheria inafuatwa hasa wanapokamata majangili na Mifugo ndani ya hifadhi zetu tunazosimamia.
Sanjari na hilo ametoa ufafanuzi kwa watumishi kuhusu mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali katika Taasisi za Uhifadhi zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuboresha utendaji.
Ametaja Baadhi ya mabadiliko hayo ni pamoja na Mabadiliko ya Kifungu cha 10 cha Sheria Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kupitia Sheria za marekebisho mbalimbali Na. 02 ya mwaka 2020 ambayo imeanzisha rasmi Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu (Wildlife and Forest Conservation Service – WFCS).
Kufuatia mabadiliko hayo, Wizara kwa kushirikiana na Taasisi za uhifadhi inaandaa kanuni na miongozo za kutekeleza Sheria ya Jeshi la Uhifadhi.
Hivyo, aliwataka watumishi kubadilika kutoka mfumo wa kiraia na kuishi kwa kufuata taratibu za kijeshi.
Pia Sheria imetoa baadhi ya mamlaka kwa watumishi ikiwepo ya kukamata, kupeleleza, kufanya shughuli za intelijensia na kushughulikia mashauri yanayohusisha mifugo kwa njia ya compound.
Mengine ni Mabadiliko ya jukumu la kukusanya mapato ya Serikali ambalo limehamishwa kutoka Taasisi za uhifadhi (TAWA, TANAPA na NCAA) zilizo chini ya Wizara kwenda TRA. Kufuatia badiliko hilo, Taasisi husika zitakuwa zinapokea fedha za kujiendesha kutoka Serikali kuu.
aidha Mabadiliko mengine yamefanyika katika ngazi ya Wizara ni Uanzishwaji wa Idara ya Uratibu wa Jeshi la Uhifadhi (paramilitary coordination division).
Kwa upande wao Watumishi wa TAWA Mkoani Tabora walimweleza Naibu Kamishna Nkuwi kuhusu changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwenye vituo vyao vya kazi ambazo nyingi alizitolea ufafanuzi na maelekezo namna ya kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuandaa mapendekezo mpango wa kina wa biashara wa namna ya kuiboresha bustani ya wanyamapori ya Tabora ambayo ipo katikati ya manispaa ya Tabora.
Hata hivyo aliwapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri na ya kizalendo wanaoyoifanya ya kusimamia raslimali ya wanyamapori kwa uaminifu kwa niaba ya watanzania.
0 comments:
Post a Comment