Katibu Mkuu Kilimo Bwana Gerald Kusaya baada ya kukata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa jengo jipya la maabara wengine karibu wakipiga makofi ni pamoja na Mtendaji Mkuu (ASA) Dkt. Sophia Kashenga pamoja na Mwenyekiti wa Bodi (ASA) Dkt. Ashura Kihupi pamoja na Wageni waalikwa na Watumishi wa Wakala wa Mbegu za Kilimo, Morogoro leo jioni tarehe 13 Oktoba, 2020.
Katibu Mkuu Kilimo
Bwana Gerald Kusaya akifungua jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa jengo jipya
la maabara wengine karibu wakishuhudia ni pamoja na Mtendaji Mkuu (ASA) Dkt.
Sophia Kashenga pamoja na Mwenyekiti wa Bodi (ASA) Dkt. Ashura Kihupi pamoja na
Wageni waalikwa pamoja na Watumishi wa Wakala wa Mbegu za Kilimo, Morogoro leo
jioni tarehe 13 Oktoba, 2020.
Katibu
Mkuu Kilimo Bwana Gerald Musabila leo jioni, tarehe 13 Oktoba, 2020 amezindua
maabara ya kisasa iliyojengwa kupitia Mradi wa Kuongeza Tija na Uzalishaji kwenye
zao la Mpunga (ERPP) kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Wakala wa Mbegu za
Kilimo (ASA) mjini Morogoro.
Akizungumza
kabla ya kuzindua maabara hiyo; Katibu Mkuu Gerald Musabila Kusaya amesema
jengo la maabara hiyo ni moja ya kazi nzuri iliyofanyika chini ya usimamizi wa
Wizara ya Kilimo na hatimaye maabara hiyo iko tayari kuanza kutumika.
Katibu
Mkuu amesema licha ya kuizindua maabara hiyo; Kuna vifaa vingine ambavyo
vinapaswa kununuliwa ili kuiwezesha maabara hiyo kufanya kazi kwa ufanisi na
kwamba Wizara itanunua vifaa hivyo mapema iwezekanavyo.
Katibu
Mkuu Kusaya amesema suala la kuongeza tija na uzalishaji katika kilimo ndiyo
limesukumu sehemu kubwa ya mabadiliko ya kiutendaji katika maeneo mbalimbali
ambapo; Ili taifa liongeze uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula yanaenda
sambamba na matumizi ya mbegu bora pamoja na pembejeo nyengine.
“Suala
la kuongeza uzalishaji wa mbegu bora ni suala la msingi hasa kipindi hiki
ambacho mahitaji na matumizi ya mbegu bora za kilimo, yameongezeka kwa kiasi
kikubwa. Hata hivyo, bado kasi ya uzalishaji wa mbegu ni ndogo.”
Aidha;
Katibu Mkuu ametoa rai kwa Watumishi wa Wakala wa Taifa wa Mbegu za Kilimo
kuendelea kutoa huduma ya kuzalisha mbegu bora za mazao ya kilimo licha ya
kukabiliana na changamoto kadhaa.
“Nafahamu
changamoto nyingi zilizopo na mnazopitia kama Wakala wa Serikali lakini bado
mnahitaji kuongeza juhudi, kasi na ufuatiliaji ulio makini katika suala zima la
uzalishaji wa mbegu bora ili ziwafikie na kubadilisha maisha ya wakulima wetu.
Dhamana hii mliyopewa ni kubwa na usimamizi wake lazima uendane na kufanya kazi
kwa kujituma na kwa uadilifu wa hali ya juu. Kufanya kazi ASA ni sawa na
kufanya kazi benki kwani fedha zipo na unazishika kila siku lakini sio zako.”
Amekaririwa Katibu Mkuu.
Wakati
huohuo, Katibu Mkuu Kusaya ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Watumishi wa Wakala
wa Mbegu Bora (ASA) kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na uhadilifu mkubwa.
“Ndugu
zangu, napenda niwahimize kila Mtumishi afanye kazi kwa uhamimifu mkubwa;
Binafasi uwa nachukia sana wizi wa mali za umma, matumizi mabaya ya rasilimali
za umma. Niwaomba tufanye kazi na atakayekataa kufanyakazi kwa uadilifu;
Tutamchulia hatua.
Baadae
Katibu Mkuu alielekea kwenye kuzindua rasmi maabara hiyo kwa kukata utepe kama
ishara ya kuzinduliwa rasmi kwa jengo hilo la maabara.
Baadae
Katibu Mkuu alikabidhi matrekta makubwa mawili kwa ajili ya kuongeza eneo la
kilimo cha mashamba ya ASA. Matrekta hayo yana uwezo wa HP 95 na ni aina ya
Valtra kutoka nchini Brazil yote yakiwa na thamani ya shilingi milioni 273.6.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo, Dkt. Sophia Kashenge amesema
kuongezeka kwa matrekta hayo mawili; Kunaifanya ASA kuwa na matrekta matano (5)
na kwamba matrekta hayo; yatachangia katika kuongeza uzalishaji wa mbegu bora
mara dufu.
0 comments:
Post a Comment