METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 15, 2020

DKT MABULA: JPM ANAYAISHI MAONO YA MWL JK NYERERE KWA VITENDO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli anaishi na kutembea katika maono na fikra za Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati yenye manufaa kwa wa Tanzania wote sanjari na kuwa na Serikali inayojali maslahi ya wanyonge.

Hayo yamebainishwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya wa kwanza wa wilaya ya Butiama ambae pia ni Naibu Waziri wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Dkt Angeline Mabula wakati wa kushiriki ibada ya misa  maalum ya kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Bikira Maria Damu ya Azizi Parokia ya Butiama Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma ambapo amefafanua kuwa pamoja na kupita zaidi ya miaka 21 bila uwepo wake lakini nchi imepata kiongozi mkuu Rais Mhe Dkt John Magufuli mwenye kuishi matamanio ya baba wa taifa ambapo shughuli nyingi alizotamani kuzifanya zimeweza kutekelezwa  ikiwemo kuhamishia makao makuu ya Serikali katikati ya nchi mjini Dodoma, kujenga mradi mkubwa wa uzalishaji umeme  katika maporomoko ya mto Rufiji unaojulikana kama Stieglers Gorge ambao unatazamiwa kuzalisha megawati 2,000 za umeme, hatua ambayo inaelezwa kuwa itasaidia kupunguza tatizo la nishati hiyo muhimu kiuchumi na kijamii.

‘.. Ni  miaka 21 sasa bila uwepo wa Mwalimu, Lakini ninavyoona ni kama bado yupo, Bado anaishi maana maono yake mengi hasa baada ya kumpata Dkt John Magufuli mambo mengi anayoyafanya yalikuwa katika maono ya baba wa taifa ..’ Alisema

Aidha Dkt Mabula akaiasa jamii kutunza amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu kama ambavyo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa akisisitiza juu ya utunzaji wa amani na kuishi kwa umoja na upendo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com