METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 24, 2020

DKT MABULA: ARDHI NI MALI, UKIITUNZA ITAKUTUNZA

Wananchi wametakiwa kuitunza na kuiongezea thamani ardhi  kwa kuhakikisha wanaipima na kuimiliki kisheria ardhi yao. 

Rai hiyo imetolewa na mgombea wa nafasi ya ubunge Jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa kata ya Kitangiri katika viwanja vya minazi mitatu ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni katika kipindi Cha lala salama kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuliongoza Jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa oktoba 28, ambapo amewaasa wananchi hao kutumia ardhi kwa shughuli za uzalishaji mali kwa kuikopea benki ili kupata mitaji ya biashara mbalimbali, kupima na kumilikishwa ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima

'.. Ardhi ni mali ukiitunza itakutunza, Na Kama mnavyojua wengi tulikuwa tumejenga bila utaratibu lakini alivyoingia Dkt Magufuli akaridhia tuwapimie na tuwarasimishie muweze kukaa kwa amani, itumieni vizuri ardhi yenu ..' Alisema

Aidha Dkt Mabula akaongeza kuwa katika kipindi Cha Serikali ya awamu tano migogoro mingi iliyokuwa ikiikabili wilaya ya Ilemela imetatuliwa ikiwemo ule wa kata ya Kirumba Kigoto Kati ya wananchi na jeshi la polisi, kata ya Kahama Kati ya wananchi na jeshi la wananchi na mingine iliyohusu taasisi kwa taasisi, taasisi na wananchi, wananchi kwa wananchi huku akiwasisitiza wananchi wa kata hiyo kuhakikisha wanalipia hati kwani zaidi ya viwanja 3273 vimepimwa lakini Kati yao 1143 pekee ndio waliochukua hati.

Akimkaribisha mgombea huyo, Meneja kampeni Kazungu Safari Idebe mbali na kufafanua juu ya miradi mikubwa ya maji iliyotekelezwa ndani ya Jimbo hilo ikiwemo Tanki la maji Ibanda, Tanki la maji Nyamhongolo, Tanki la maji Nyasaka akawataka wananchi hao kuchagua wagombea wa CCM  kwani ndio wenye uwezo wa kutatua kero na changamoto zao pamoja na kuwasisitiza kutojaribu kuchagua wagombea wa upinzani kwani kufanya hivyo ni kuyakataa maendeleo.

Kwa upande wake mgombea wa udiwani wa kata hiyo kupitia CCM Ndugu Donarld Ndaro akawahakikishia wananchi hao kuwa anazitambua changamoto zao na anao uwezo  wa kuzitatua hivyo kuomba wamuamini na wampigie kura nyingi za ndio yeye, Mbunge wa CCM na Rais ili ikawe rahisi kwake kutatua kero zao.

Katika mkutano huo  uliohudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mnec Richard Bundala, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela Nelson Mesha, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake mkoa wa Mwanza Bi Hellen Bogohe, wabunge wateule wa viti maalum wanawake Bi Furaha Matondo, Kabula Shitobelo, na Mbunge aliyemaliza muda wake Bi Maria Kangoe wakapata wasaa wa kuwaombea Kura wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu kwa mwaka huu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com