Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wajumbe wa Menejiment ya Wizara hiyo leo Ihumwa jijini Dodoma wakati anawaaga kuanza ziara ya kutembelea mradi ujenzi wa Reli ya ya Kisasa (SGR) ili kujionea maendeleo yake ikizingatiwa Wizara hiyo ndiyo yenye dhamana kuisemea Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika wakitembelea handaki la nne eneo la Kilosa mkoani Morogoro kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaojengwa kutoka Dar es Salaam hadi mkoani Mwanza.

Muonekano wa moja ya mahandaki itakapokuwa inapita Reli ya Kisasa (SGR) eneo la
Kilosa Mkoani Morogoro.
Ujenzi
wa Reli ya ya Kisasa (SGR) nchini unalenga kuleta maendeleo ya watu kwa
kurahisisha muda wa usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo ambapo kutoka
Dar es Salaam hadi Morogoro itakuwa ni saa tatu au dakika 90 hatua
itakayopunguza muda mwingi unaopotea barabarani na kuwafanya wananchi kuwahi
kufanyakazi nyingine za maendeleo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali
Dkt. Hassan Abbasi amesema hayo leo Ihumwa jijini Dodoma wakati anawaaga
Menejimenti ya Wizara hiyo kuanza ziara ya kutembelea mradi wa SGR ili kujionea
maendeleo yake ikizingatiwa hiyo ndiyo ni Wizara yenye dhamana kuisemea
Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).
“Wizara
ya Habari ni Wizara muhimu sana katika nchi yetu na mradi huu pia. Ndiyo wizara
yenye dhamana na habari kwa maana hiyo tumekuwa tukiutangaza sana, na
kuukiulinda mradi huu ili kuwaonesha watanzania nini kinaendelea kwenye huu
mradi” alisema Dkt. Abbasi.
Dkt.
Abbasi amesema kuwa Tanzania ipo makini kuwekeza kwenye mambo ambayo ni muhimu
katika kuleta manufaa na maendeleo ya watu na kusisitiza kuwa ni utamaduni mpya
kwenye nchi yetu kuwa na taifa la wachapakazi, kuwa watanzania wanaojiamini na
kuwa watu wanaopenda mambo mazuri ambayo yanaletwa na Serikali kwa manufaa ya
wananchi wake.
“Tunaposema
huu ujenzi wa reli ni kitu, ndiyo ni kitu, reli ya SGR ni kitu kinachokwenda
kuleta maendeleo ya watu. Utakapoweza kusafiri kwa saa tatu au dakika 90 Dar es
Salaam hadi Morogoro umepunguza muda mwingi wa kupoteza barabarani na kuwahi
kwenda kufanyakazi”alisisitiza Dkt. Abbasi.
Mradi
huo ni moja miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali nchini na kuwa miongoni
mwa miradi mikubwa Afrika ambapo Serikali imewekeza trakriban trilioni saba
(07) kwa kipande cha Dar es Salaam, Morogoro hadi Mkutupora mkoani Singida
ambapo kipande cha Morogoro hadi Dodoma kimefikia asilimia 42 hadi kukamilika
kwake.
Akitoa
maelezo ya mradi huo kwa mwajumbe wa menejimenti ya wizara hiyo, Meneja wa
mradi kipande cha Morogoro hadi Mkakutupora mkoani Singida Mhandisi Mteshi Tito
amesema reli hiyo itatumiwa na treni ya abiria ambayo itakuwa na mwendo wa kasi
ya kilometa 160 kwa saa na ya mizigo itatumia saa moja kwa kilometa 120 hatua
inayopelekea mradi huo kuwekewa uzio kuanzia mwanzo hadi mwisho ili kuepusha
muingiliano wa watu wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Mhandisi
Mteshi ameongeza kuwa kipande cha reli ya SGR kati ya Morogoro na Mkutupora
Singida kina jumla ya km 422 ambapo km 336 zinajumuisha njia kuu na km 86
sehemu za kupishania treni.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema Menejiment ya Wizara hiyo imeshuhudia na kujionea wenyewe uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali na kuongeza itakapokamilika reli hiyo kutakuwa na usafiri wa uhakika kutoka Dar es Salaam hadi Mkutupora Singida ambayo itakuwa na manufaa kiuchumi katika sekta ya usafirishaji.
0 comments:
Post a Comment